Mwandishi Wetu

Hukumu ya kesi ya madai ya mwanamuziki Lameck Ditto dhidi ya kampuni ya Multchoice Tanzania Limited maarufu DSTV itatolewa Julai 16.

Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Bwakeya alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam mwaka 2020 akiiomba Mahakama hiyo iamuru kampuni Multichoice Tanzania imlipe fidia ya Sh 6bilioni kwa kutumia wimbo  wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake wakati wa kampeni za  fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019.

Pia ameiomba Mahakama iamuru alipwe Milioni 200 kutokana na madhara ya jumla, pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo akidai kampuni hiyo imemnyima fursa ya kunufaika na kazi yake.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jaji mfawidhi, Salma Maghimbi, imekamilisha ushahidi wa pande zote, Ditto akileta mashahidi watano na DSTV ikiwa na mashahidi wawili, Astrid Mapunda na Johnson Mshana.

Upande wa Ditto, baadhi ya mashahidi wake walikuwa ni produzya wa wimbo huo, Emmanuel Maungu (Emma the boy), meneja wa Ditto,  Rodney Rugambo na Angela Karashani.

Upande wa Ditto unatetewa na mawikili, Ally Hamza na Elizabeth Mlemeta wakati DSTV inatetewa na mawakili, Simon Lyimo naThomas Mathias.

Nje ya Mahakama, mmoja wa mawakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta alisema Juni 24, watawasilisha hoja za mwisho au uchambuzi wa mawakili kuhusiana na ushahidi au utetezi uliotolewa na kusubiri hukumu Julai 16.

"Juni 24 tunafile closing submissions (mawasilisho ya hoja za mwisho)," alisema Elizabeth.

Wakili wa DSTV, Thomas Mathias (aliyebeba begi kushoto) na wakili wa Ditto, Ally Hamza (aliyebeba begi kulia) wakiteta jambo wakiwa wanashuhudiwa na Lameck Ditto (wa kwanza mbele), wakili mwingine wa DSTV, Simon Lyimo (mwenye koti nyuma) na wakili wa Ditto, Elizabeth Mlemeta. (nyuma kulia)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...