Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

SERIKALI Ya Ufaransa kupitia Ubalozi wake wa Tanzania umedhamiria kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania pamoja na sekta binafsi katika kufanya biashara na uwekezaji wenye tija na hiyo ni pamoja kutoa mafunzo kwa watanzania watakaofikiwa na miradi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa hafla maalum ya kuwapokea wafanyabiashara na wawekezaji hao wa kampuni zipatazo 27 kutoka Ufaransa iliyofanyika katika Ubalozi huo jijiji Dar es Salaam Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui ameeleza kuwa, ujio huo umedhamiria kufanya biashara yenye tija na manufaa kwa mataifa hayo mawili katika sekta mbalimbali ikiwemo nishati, kilimo, maji, ukuaji wa miji na utunzaji wa miti ambapo tayari TFS na kampuni ya Tyllium kutoka Ufaransa wamesain hati ya makubaliano katika utunzaji wa mazingira ikiwemo kuulinda mlima Kilimanjaro.

Amesema tayari kampuni za Ufaransa zimeonesha nia thabiti za kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanja vya ndege na reli ya kisasa.

Balozi Hajlaoui amesema, ugeji huo ujio pia utatembelea visiwani Zanzibar na kukutana na wafanyabiashara na kujadili fursa na maeneo muhimu ya kushirikiana na kuanza utekelezaji wake.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Mwadini ameeleza kuwa wafanyabiashara na wawekezaji hao wametoka kwenye kampuni kubwa zenye uzoefu na teknolojia ya kutosha.

“Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan nchini Ufaransa ni matokeo ya ujio huu na wamekuja hapa kutokana na uwepo wa mazingira rafiki na wezeshi ya biashara na uwekezaji, rasilimali, soko kubwa ndani na nje ya Nchi pamoja na utulivu….Ubalozi utaendelea kushirikiana na kutafuta fursa zaidi za biashara na uwekezaji ili watanzania waweze kunufaika za uhusiano huu.” Ameeleza Balozi Mwadini.

Pia Mkuu wa msafara wa wafanyabiashara hao Phillipe Labonne amesema, ujio huo ulivutiwa na namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alivyotangaza fursa zilizopo katika ziara yake nchini Ufaransa.

“Tumekuwa na majadiliano yenye tija katika kubainisha fursa na kuanza kushirikiana, Tumefanya kazi na kampuni za Tanzania kwa mafanikio …. Tutarudi tena Tanzania na kushirikiana katika sekta mbalimbali hususani nishati, elimu, kilimo na uhandisi na katika soko Tanzania is a country of corridors ina soko kubwa ndani na nje ya nchi tunaamini mataifa haya mawili yatanufaika na ushirikiano huu.” Amefafanua.

Aidha amesema kuwa katika ushirikiano huo watatoa mafunzo kwa wananchi watakaonufaika na miradi mbalimbali ili waweze kuiendesha huku wakimpongeza Balozi Nabil kwa kuiwakilisha vyema Ufaransa nchini Tanzania kwa kuanzisha program mbalimbali za mafunzo kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana.
 

Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Nabil Hajloui akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla maalum ya kuwakaribisha wageni hao iliyofanyika katika makazi ya Ubalozi, Nabil amesema uthubutu wa mataifa hayo mawili ni matunda ya ujio wa kampuni 27 nchini. Leo jijini Dar es Salaam.



 

Matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
 

Mkuu wa msafara wa ugeni huo Phillippe  Labonne  akizungumza wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa sera mathubuti na utulivu vimewavutia kuja kuwekeza Tanzania. Leo jijini Dar es Salaam.
 

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Ali Mwadini akizungumza wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa wataendelea kuonesha ushirikiano katika kuhakikisha watanzania wananufaika na ushirikiano huo. Leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...