KUELEKEA Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani inayoadhimishwa Mei 20 kila mwaka, Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA,) imeendelea kuwafikia wadau mbalimbali na kutoa elimu na kuwakumbusha masuala mbalimbali yanayohusu vipimo ikiwemo uzingatiaji wa sheria za vipimo pamoja na afya.

Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Sterio, Temeke jijini Dar es Salaam Meneja wa WMA Mkoa wa Temeke Gaspar Matiku amesema, katika kuelekea kuadhimisha siku hiyo iliyobebwa na kauli mbiu ya ‘Tunapima Leo kwa Kesho Endelevu’ WMA imekuwa ikikutana na wadau mbalimbali na kutoa elimu na kukumbushana juu ya uzingatiaji wa sheria za vipimo pamoja na afya kwa ujumla.

“Vipimo pia ni pamoja na afya zetu hususani wabebaji, mtu ana kilo 60 anabeba gunia la kilo 100 au 150 kwa kujali afya za wabebaji bidhaa zinaweza kufungwa kwa kilo za wastani….Kwa kauli mbiu ya Mwaka huu ya ‘Tunapima Leo kwa Kesho Endelevu, ukimbebesha zaidi ya kilo 100 sio kwa maendeleo endelevu na afya pia.” Amesema.

Matiku amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia sheria za vipimo ikiwemo uhakiki wa mizani kwa usahihi pamoja na vifungashio kwa kuhakikisha kifungashio kimoja hakizidi kilo 100 ili kuepukana na faini kwa kuzidisha mzigo.

“Sheria inasisitiza uhakiki wa mizani ili itende haki kwa usahihi, mafungu, makopo na madebe sio rasmi mnaweza kukosa thamani ya bidhaa kwa kutotumia vipimo halisi kwa kuwa havijahakikiwa na pia inapelekea mazingira ya udanganyifu……Tuhame tutumie mizani kuliko kukadiria katika mafungu.” Ameeleza.

Kuhusiana na ufungashaji wa mizigo hususani inayotoka kwa wakulima Matiku amewataka wafanyabiashara hao kuwa na mizani binafsi pamoja na kuwaelimisha wakulima kuwa na mizani ili kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuwa kila kilo inayozidi haitozwi na mkulima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko la Sterio Temeke Rashid Milao ameishukuru WMA kwa kutoa elimu hiyo kwa vitengo 21 vya wafanyabiashara wa soko hilo ambayo imewachakata upya na itawasaidia kufanya vizuri zaidi katika masuala ya vipimo.

Ameiomba Serikali kupitia WMA kupitia sheria hususani katika ushuru kwa kutotoza kwa gunia bali kutumia mizani na kuwataka wafanyabiashara kupitia sheria walizopewa na kuzizingatia ili kufanya biashara kwa uhuru.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mafunzo hayo baadhi ya wafanyabiashara hao wameipongeza WMA kwa kuwafikia na kutoa elimu na kushauri kutoa elimu hiyo kwa wanunuzi ambao pia hawana uelewa wa vipimo hususani mizani kwa kuwa wateja wengi huchagua mafungu kwa kutoamini mizani.
 

Meneja wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA,) Mkoa wa Temeke Gaspar Matiku akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Sterio Temeke kuhusu maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani ambayo WMA inaiadhimisha kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali. Leo jijini Dar es Salaam.
 

 Meneja wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA,) Mkoa wa Temeke Gaspar Matiku akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na wafanyabiashara wa soko la Sterio jijini Dar es Salaam.

 

Matukio mbalimbali wakati wa mafunzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...