MBUNGE  wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe, Abdulaziz M. Abood ameendele na zoezi lake la kurekebisha miundombinu ya Barabara korofi katika baadhi ya Kata zilizopo kwenye Jimbo lake kama sehemu ya kufufua njia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wananchi wa Jimbo hilo kufuatia kuharibiwa vibaya kwa miundombinu hiyo wakati wa mvua kubwa zilizoisha hivi karibuni.

Mhe Abood ameendelea na zoezi la ukarabati wa Miundombinu ya Barabara ambao ulianza Apliri 04 hadi 08 Mwaka huu katika Kata za Chamwino na Kiwanja cha Ndege na baadae Kata ya Tungi Apliri 17 hadi 21 na kisha kusimama kwa muda kwa ajili ya kupisha Mvua kubwa ambazo kwa sasa zinaelekea ukingoni, hivyo kuendelea na zoezi hilo Mei 10 hadi 16 Mwaka Mwaka huu Jimboni humo.

Kata zilizofikiwa na muendelezo huo ni pamoja na Kata ya Kihonda, barabara ya inayoelekea katika Hospitali ya Wilaya ya Morogoro, Kata ya Lukobe barabara ya Tushikamane kwa wagogo, Lukobe juu Transformer na Mtaa wa Mbuyuni kwenye Kata hiyo katika Barabara ambazo ziliharibiwa na Mafuriko yalitokea Januari 13 Mwaka huu.

Aidha, Mhe Abood kwa kutumia gharama zake binafsi amerekebisha pia barabara za Kata ya Kihonda Maghorofani Mei 12 Mwaka huu, ambapo katika Kata hiyo Mhe Abood amerekebisha Barabara za Idiva – Ahmadiyyah, Barabara inayotoka Njia kuu ya Dodoma kuingia katika Shule ya Msingi ya Mtakatifu ANNA, Barabara ya Soko kuu la Kata hiyo pamoja na Brabara ya Kuu ya Idiva.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe Abood Mei 13 Mwaka huu akiwa katika Kata ya Kichangani amerekebisha barabara ya Sabato, Barabara ya Oil com na Barabara ianayounganisha Mtaa wa Area five na Barabara kuu ya Kichangani ili kusogeza na kurejesha huduma za kimsingi katika jamii kwa kurahisisha upitaji wa barabara hizo kwa wananchi.

Sanjari na hayo, Mhe Abood katika kuhitimisha uchongaji wa barabara kwa awamu ya pili, Mei 14 Mwaka huu, amerekebisha barabara inayotoka njia kuu ya Dar es salaam ianyofahamika kama Barabara ya Uhamiaji nayo imerekebishwa kwa wananchi na wakazi wa Kata ya Mafisa hadi eneo la kutupia maji taka. Barabara ambazo hazikuwa zinapitika vema kabla ya marekebisho hayo.

Wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa nyakati tofauti wameonesha kufurahishwa na wameshukuru sana Mhe Abood kuhusiana na Ukarabati wa Barabara hizo ambazo zinawasaidia kuendelea na Maisha yao ya kawaida kwa kupata nafasi ya kupita kutoka sehemu moja kwenda nyingine bila ya changamoto yoyote, hivyo kumuomba Mhe Abood aendelee hivyo katika Kata zingine kwa lengo la kutoa huduma faafu kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...