*Ugunduzi umetokana na yeye mwenyewe kuwa na changamoto ya usikivu hafifu

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV Tanga
MWALIMU wa VETA Kigoma Innocent Maziku agundua kifaa cha kuongeza usikivu kutokana na yeye mwenyewe kuwa na usikivu hafifu.

Maziku amebainisha hayo katika Banda la VETA katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu ya Ubunifu na Ujuzi yanayoendelea katika Viwanja Vya Shule ya Popatlal Mjini Tanga.

Amesema kuwa wakati anasoma aligundua ana changamoto ya usikivu hafifu hali hiyo ilifanya kuwa na wakati mgumu wa kusoma kwake hususani katika kumsikiliza mwalimu.

Amesema kidato cha kwanza hadi cha nne akafaulu kwenda kidato cha tano na sita akafaulu kwenda Chuo huku hiyo hali anayo ya usikivu.

Maziku amesema wakati amepata ajira ya Ualimu Kigoma baada ya muda akaanza kubuni kifaa cha kuongeza usikivu kwa mara ya kwanza hakufanikiwa lakini mara ya pili aliongeza mashine za kuongeza wawimbi ya sauti 'Microphone' manne na alivyojaribu akauna anapata usikivu vizuri.

Amesema katika mazingira hayo alitokea mwingine mwenye changamoto hiyo ya usikivu hafifu alivyoweka nae akawa anasikia.

Amesema kwa hatua hiyo kifaa hicho anatumia mwenyewe huku akijua wapo baadhi ya watu wanachangamoto hiyo.

Hata hivyo amesema kuwa kilichobaki ni baadhi ya taasisi kuweza kupima ubora na ndipo kazi yake atengeneze kwa ajili ya kusaidia jamii.

Maziku amesema kuwa na ubunifu ambao unakuwa hauendelezwi unafanya jamii kubaki na changamoto zile zile.

"Natamani kifaa hiki kitumike hata kusaidia jamii yangu ambayo ina changamoto usikivu hafifu ili waweze kusikia"amesema Maziku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...