Na Mwandishi wetu, Dodoma

Serikali imetangaza kuanza ujenzi wa Makumbusho ya Marais katika jiji la Dodoma ili kuhifadhi historia ya waasisi na viongozi wakuu wa nchi ya Tanzania.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameyasema hayo bungeni leo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2024/25.

Mhe. Kairuki amesema kuwa ujenzi huo unalenga katika kuongeza wigo wa uhifadhi wa urithi wa asili na utamaduni wa Mtanzania.

Amesema Makumbusho ya Marais yataimarisha na kuhamasisha tafiti za masuala ya historia pamoja na kuongeza vivutio vya utalii vya utamaduni.

Amesema ujenzi huo utakuwa chini ya taasisi ya Makumbusho ya Taifa la Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...