Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Mhandisi Asajile John ambaye ni Meneje Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya kati amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Tanzania imejiimarisha kama kitovu cha Mawasiliano ya Posta Kufuatia kufunguliwa kwa kituo cha Kimataifa cha Teknolojia ya sekta hiyo na Ofisi ya Kanda ya Umoja wa Posta Ulimwenguni (UPU) Jijini Arusha ambayo ilizinduliwa September 2023.

Na kuongeza kuwa Tanzania imeweka miundombinu muhimu ya huduma za posta zinazowezeshwa na ubunifu ,ikiwa ni pamoja na mfumo wa anwani za makazi na postikodi ambao uanatarajiwa kuwezesha ufukishaji na uchukuaji vitu vinavyonunuliwa na kuhitajika kufikishwa kwenye makazi au ofisi za wahusika.

Mhandisi John ameeleza hayo mapema leo hii May 22,2024 Jijini Dodoma katika mkutano wake na Wanahabari wakati akielezea Mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Mawasialiano.

"Kipandi hiki cha uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan pia kimeshuhudia Tanzania ikijiimarisha kama kitovu cha Mawasiliano ya Posta Afrika kufuatia kufunguliwa kwa kwa kituo cha Kimataifa cha teknolojia ya sekta ya hiyo na ofisi Kanda ya Umoja wa posta Ulimwenguni (UPU) Jijini Arusha lililofunguliwa na Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan September 2023. Kituo hicho na Ofisi hiyo vitakuwa kwenye jengo la kisasa la Umoja wa posta Afrika (PAPU),ambalo limejengwa kwa ubia wa Serikali ya Tanzania na Umoja huo".

"Tanzania imeweka miundombinu muhimu ya huduma za posta zinazowezeshwa na ubunifu,ikiwa ni pamoja na amfumo wa anwani za makazi na postikodi ambao unatarajiwa kuwezesha ufikishaji na uchukuaji vitu vinavyonunuliwa mitandaoni na kuhitajika kufikishwa kwenye makazi au ofisi za wahusika".

"Katika kipindi cha mwezi Januari hadi March 2024 takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na ongezeko la watoa huduma za posta na usafirishaji wa Vifurushi na Vipeto kutoka 117 mwezi Desemba 2023 hadi kufikia 134 mwezi Machi 2024".

Wakati huo huo pia ameongelea suala la ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu na Intaneti kwa laini za simu,Akaunti za pesa na Miamala ya Pesa ambapo amesema wakati usajili wa laini za simu umeongezeka kwa wastani wa asilimia 3.1 kati ya Desemba 2023 na Machi 2024, usajili wa akaunti za fedha kidigitali uliongezeka kwa wastani wa asilimia 0.02.

"Vidokezo vya ukuaji wa sekta vinaonesha mabadiliko ya kasi kwenye maeneo mengi hususani katika usajili wa akaunti za pesa ambapo takwimu za mwezi machi 2024 zinaonesha usajili wa akaunti hizi umefikia 53,013,385 kulinganisha na usajili wa akaunti 52,875,129 mwezi Desemba mwaka 2023. Hii inaashiria kwamba watumiaji wengi wa simu za mkononi wanajisajili kwa huduma za fedha mtandaoni na kwa njia ya kidijiti".

"Wakati usajili wa laini za simu umeongezeka kwa wastani wa asalimia 3.1 kati ya Desemba 2023 na Machi 2024,usajili wa akaunti za fedha kidijitali uliongezeka kwa wastani wa asilimia 0.02".

"Laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka 70,292,899 Desemba 2023 hadi 72,496,095 mwezi Machi 2024. Ongezeko hili ni kutokana na unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma".

"Miamala ya kifedha kupitia sumu za mkononi Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano kutoka bilioni 3 mwaka 2019 hadi bilioni 5.3 .waka 2023 ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 19 ndani ya mwaka mmoja ,hali inayoakisi kukua kwa mfumo jumuishi wa kifedha Nchini".

TCRA inatoa leseni kwa watoa huduma za simu za mkononi na kuwapa namba za mawasiliano na misimbo au namba fupi ya kuwezesha Miamala hiyo. Benki kuu ya Tanzania inasimamia sekta ya fedha kwa ujumla na inatoa leseni za huduma za fedha mitandao. Hivyo Taasisi hizi zinzshirikiana kwenye masuala ya fedha mtandaoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...