NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BENKI ya Biashara (TCB) kwa kushirikiana na Kampuni ya Metro Life Assuarance wamezindua bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma zake za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambayo inawapa usalama wa kifedha pamoja na kuleta ndoto na matarajio kwa wateja wao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware amesema ubia baina ya TCB Benki na kampuni ya bima ya Metro Life Assurance unafungua ukurasa mpya wa usalama kifedha na utulivu wa wateja ambao wanakabidhi kesho yao mikononi mwa wadau hawa wawili.

Aidha akizungumzia kuhusu huduma ya ADABIMA amesema ni huduma maalumu kwa ajili ya ada ya shule inayokamilisha kiu ya mzazi au mlezi kumwona mtoto wake akifanikiwa kwa kupata elimu bora anayostahili na bidhaa hiyo ilithibitishwa na Mamlaka mnamo tarehe 22 Novemba 2023.

Amesema, ADABIMA ni suluhisho la changamoto za maisha lakini pia ni ahadi kwa wateja kwamba lolote litakalotokea kampuni yake itasimama pamoja naye kuhakikisha kwamba mtoto anasoma na kuhitimu masomo yake bila kadhia yoyote ile.

Kuhusu Saccoss Schemes Credit Life Insurance, Dkt. Saqware amesema ni bima maalumu kwa ajili ya wadau wa vikundi hivi. "Tunatambua changamoto wanazopitia watoa mikopo hawa na wapewa mikopo ukizingatia uwepo wa tofauti ndogo kati ya fursa na uwezekano wa kupata hasara".Pamoja na hayo ameeleza kuwa Mamlaka itahakikisha huduma hiyo inaendelea kuwapa watumiaji usalama wa kifedha, utulivu, kujiamini na amani. "Wadau hawa wanajenga kesho iliyo bora kwa kuinua uwezo wa watoa mikopo na kuwahakikishia wakopaji usalama na umiliki wa mali zao endapo watashindwa kulipa".

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya TCB, Jema Msuya amesisitiza kuwa lengo la kuja na mpango huo ni kutoa uendelevu wa elimu kwa watoto ikiwa wazazi watapata majanga ya kifo ama ulemavu wa kudumu na kumfanya ashindwe kulipa ada ya shule

Naye Mkuu wa Kitengo Cha Bima kutoka TCB, Francis Kaaya amebainisha kuwa mpango huo utasaidia watoto kufikia malengo yao kimasomo ikiwa wazazi wao watapata majanga .

"Tunaelewa umuhimu mkubwa wa elimu katika kujenga kesho bora ya jamii yetu.Bima hii inawapa usalama wa kitengo cha fedha lakini pia inalea watoto". Amesema kaaya

Pia kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Metro Life Assurance, Amani Boma amesema kupitia ushirikiano wao na Benki ya TCB wanajivunia kuwaletea watanzania huduma ya Bima kadri ya mahitaji yao lakini pia kuvisaidia vikundi vya huduma ndogo za fedha.

“Tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na SACCOS pamoja na Vikundi vya huduma ndogo za fedha (micro-finance) katika kuimarisha uchumi na jamii yote nchini, kupitia ushirikiano wetu na TCB Benki tunajivunia kuwaletea Watanzania huduma ya bima kadiri ya mahitaji yao na pia kuvisaidia Vikundi vya huduma ndogo za fedha.”. Amesema 

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware akiwa pamoja na viongozi wa Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance mara baada ya kuzindua bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware akionganisha baadhi ya maumbo ya maneno kuashiria kuzindua bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya TCB, Jema Msuya akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo Cha Bima kutoka TCB, Francis Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Metro Life Assurance, Amani Boma akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya Benki Bima kupitia huduma za ADABIMA na Saccos Schemes Credit Life ambapo Benki ya TCB pamoja na Kampuni ya  Metro Life Assuarance kufanikisha uzinduzi huo leo Mei 11,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...