Na. Damian Kunambi, Njombe.

Serikali Imeoa fedha kiasi cha Sh. Mil. 800 kwaajili ya ujenzi wa soko la samaki katika kata ya Manda Wilayani Ludewa mkoani Njombe litakalo wezesha wavuvi wa ziwa Nyasa na wafanyabiashara wanaouza samaki kufabya biashara pasipo wasiwasi wa kuharibikiwa.

Akizungumza katia mkutano wa utambulishwaji wa mradi Mtaalamu kutoka Idara ya Miundombinu Michael Mbyalo amesema ujenzi wa soko hilo tayari mchakato wake umekwisha anza ambapo kuanzia sasa Mkandarasi ataleta vifaa na ndani ya wiki mbili zijazo ujenzi utaanza na unatarajiwa kukamilika Desemba 14 mwaka huu.

"Kwa utaratibu wa miradi leo tumekuja kumuonyesha Mkandarasi eneo analotakiwa kulijenga halafua kutokana na mkataba wetu atatakiwa kujiandaa kwa muda wa wiki mbili kwa kuleta vifaa mbalimbali ikiwemo kuzungushia wigo eneo la mradi kisha May 14 atatakiwa kuanza rasmi ujenzi". Amesema Mbyalo.

Naye Mkandarasi wa mradi huo kutoka katika kampuni ya Hyundavis Co.LTD amewataka wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kupata ajira mbalimbali katika ujenzi huo kwani mradi huo utawapa kipaumbele zaidi wananchi wanaozunguka mradi badala ya wanaotoka nje ya mradi huo huku katibu wa Mbunge Alphonce Mwapinga akiwataka wananchi kuulinda mradi na kutofanya uharibufu ikiwemo kuiba vifaa.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Sunday Deogratius amesema soko hilo limekuja katika muda muafaka kwani kwa sasa wanatarajia kuanza kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali ili viweze kuweka vizimba na kufanya ufugaji wa samaki katika vizimba hivyo.

"Tayari tulishafanya majatibio ya ufugaji wa vizimba na ukawa na matokeo mazuri hivyo kwa sasa tunaka wavuvi wetu wajikite katika ufugaji wa vizimba ili watakapokosa samaki katika uvuvi wa kawaida soko lisikaukiwe na samaki kwakuwa watavuliwa katika vizimba", Amesema Deogratius.

Sanjari na hilo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa jimbo la Ludewa kwa ushirikiano wao na kufanikisha kupatikana fedha hizo zitakazoenda kufanya mapinduzi ya kiuchumi wilayani humo.

Josaya Luoga ni Katibu siasa na Uenezi mkoa wa Njombe amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa mradi huo unajengwa kwa viwango vinavyo hitajika na umalizike kwa wakati huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo Stanley Kolimba akisema chama hicho ndicho chama chenye kujali wananchi wake.

Nao baadhi ya wavuvi na wafanyabiashara hao wa samaki wamepongeza hatua hiyo iliyo fikiwa na wamekuwa wakilisubiri kwa muda mrefu kwani samaki wamekuwa wakioza Kutokana na kutowauza kwa wakati na wakati mwingine hulazimika kuuza kwa bei ya chini ilimradi waishe kwa haraka.

Kukamilika kwa mradi huo utaenda kutatua changamoto za wavuvi na wafanyabiashara wa kata 8 zilizopitiwa na ziwa hilo wilayani humo sambamba na wilaya za jirani kitu ambacho kitaongeza ukuaji wa uchumi wa kata, Wilaya Mkoa na nchi kwa ujumla.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...