Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko akizunumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wanasayansi unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo  Mei 14,  hadi Mei 16, 2024 jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

SERIKALI imewataka watafiti nchini kuendelea kufanya tafiti kwa ajili ya maendeleo ya taifa pamoja na kutoa suluhisho kwenye magonjwa mbalimbali.

Imesema inatambua umuhimu na mchango wa tafiti za kisayansi katika nyanja mbalimbali ikiwemo kijamii na kiuchumi zinazochangia kuchochea maendeleo ya nchi.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameyasema hayo leo Mei 14, 2024 akimwuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango katika ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wanasayansi unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo  Mei 14,  hadi Mei 16, 2024 jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

Akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Tafiti za Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Biteko amesema Tanzania kupitia NIMR imefanya utafiti uliowezesha uzalishaji wa chanjo na dawa ziligunduliwa na wataalam wa ndani.

Amesema, Serikali inayoongozwa na Rais Samia inaamini katika tafiti za kisayansi na inaamini pia kuwa hakuna maendeleo bila utafiti na hivyo ili kupata mafanikio ni lazima tafiti zifanyike na zije na matokeo chanya.

Amesema Serikali imewekeza vya kutosha kwenye utafiti katika sekta ya afya ili kuwa na ugunduzi wa ndani ya nchi akiongeza kuwa pamoja umuhimu wa watafiti kutoka nje kuna umuhimu wa kuwa wagunduzi wa ndani.

"Ili tupate maendeleo zaidi hususani kwenye Sekta ya afya inatupasa tuwe na ugunduzi wetu wenyewe, tumeshaanza tumekuwa na dawa na chanjo zetu wenyewe ." amesema Dkt. Biteko.

Dkt Biteko amesisitiza kuwa utafiti ndio unachagiza maendeleo kwa kutoa muongozo wa kisayansi wenye uhakika .

"Maendeleo mahala popote ili yaweze kutokea lazima kuwe na utafiti wa  kisayansi, lazima kuwe na tafiti za uhakika bila tafiti tutakuwa tunabahatisha na tutakosoa".

"Serikali ya Tanzanian inaamini hakuna maendeleo bila utafiti ukitaka kufanikiwa lazima ufanye utafiti kama hufanyi utafiti huwezi kuendelea", amesema Dkt Biteko

Amesema kuwa NIMR imetoa mchango mkubwa nchini hususani katika kutoa muelekeo wa sera nzuri za afya kutokana na utafiti wao wa kisayansi wanaoufanya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Molel amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imeamua kuwekeza kwenye utafiti katika sekta ya afya ndio sababu iliyopelekea kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 6.1 kwa ajili ya tafiti ngumu.

Dkt. Mollel amesema kuwa sasa ni muda muafaka kwa Watanzania kufanya tafiti ili kuzikabili changamoto zinazoibuka duniani.

"Tufikiri siku itakapootokea janga kubwa pakatokea virusi watakao kula watu na cyber kiasi tushindwe kuwasiliana na watu wengine dunia tukabaki wenyewe hapo ndipo tunapohitaji watafiti wafanye tafiti ya jambo ambalo hawajapata kulisikia hapo ndio tujue hawa watu ni muhimu " amesema Dkt. Mollel.

Naye, Mkurugenzi wa NIMR, Profesa. Said Aboud amesema kuwa mkutano huo umekutanisha watafiti wa kisayansi kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na watafiti wa ndani watakaojadili tafiti za magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuambukiza na yasiyoambukiza .

"Leo tumekutana na wanasayansi Kukuza na kuendeleza mawazo yetu ya kiutafiti ili kupambana na maradhi haya." amesema Profesa Aboud.

Amesema kuwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile Kisukari, Shinikizo la Damu, yamekuwa tishio ulimwenguni na kwamba NIMR ina mpango maalum wa 2021 2026 wa kupambana na maradhi hayo.

Amesema kuwa mafanikio makubwa ya NIMR ni pamoja na kuaminika kimataifa pamoja na utafiti wa chanjo moja ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike.

Amesema matokeo ya chanjo hiyo yameifanya Uingereza kubadili sera zake katika sekta ya afya.

Amesema kuwa NIMR imepiga hatua kutoka kuwa na watafiti wachache hadi kufikia watafiti 734 wa kisanyansi na Vituo saba vya kiutafiti za kisayansi.

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa (NIMR), Dkt. Ntuli Kapologwe  amesema kuwa sasa hivi wanatekeleza maoni ya Mwalimu Nyerere ya mwaka 1961 alipotangaza madui watatu yaani Maradhi, Ujinga na Umasikini.

Amesema kuwa NIMR imekuwa ikifanya jitahada za kupambana na maradhi kwa kufanya tafiti mbalimbali zilitoa matokeo chanya na kuongeza kuwa watu wengi kwenye sekta ya afya wanafikiri matibabu zaidi kuliko kufikiria kukinga maradhi.

Aidha Dkt. Kapologwe ametoa rai ya kuipa nguvu NIMR ili kuongeza jitahada za kufanya utafiti juu ya kujikinga na maradhi .

Dkt. Hery Marwa amesema kuwa jamii inatakiwa kujengewa uelewa juu ya magonjwa yasiyoambukiza huku akichagiza kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni uchache wa wataalam (madaktari) kwa ajili ya kuyakabili maradhi hayo.

Amesema kuwa jukumu kubwa ni kupunguza gharama za matibabu ili kuwananchi wote kupata matibabu.
Kwa upande wake Dkt. Marry Maige Mtafiti Mwandamizi kutoka NIMR amesema kuwa tayari taasisi hiyo imefanya utafiti na kubaini kuwa mtindo wa maisha umechangia sana ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt Marry amesema kuwa mfumo wa ulaji, na mtindo wa maisha na mabadiliko ya tabianchi yamechangia ongezeko la maradhi yasiyoambukiza.

Amesema kuwa mpango endelevu wa kuyakabili maradhi (NCD) utiwezesha kupambana na magonjwa hayo.







Baadhi ya Watafiti Wanasayansi wakiwa katika katika katika ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wanasayansi unaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo  Mei 14,  hadi Mei 16, 2024 jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...