Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesem kuna umuhimu wa kuingia katika matumizi ya akili bandia ili iwasaidie kulinda uaminifu na taaluma.


Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo mawakili wa serikali ambapo amesema kasi ya kutoa huduma kwa kuwa dunia ya leo inahitaji kasi kubwa.

“Akili ya kibinadamu, mawazo ya kibinadamu pekee yake yanaweza kutuchelewesha kwa sababu dunia inakwenda kwa kasi hivyo akili bandia haiepukiki katika utendaji wetu,”alisema.

Pia amese mawakili hao wanahitaji kujenga mtandao wa ushirikiano na vyombo vingine vya kisheria, asasi za kiraia na mashirika mengine ili kuhakikisha wanaboresha mfumo wao wa sheria kwa manufaa ya wananchi wote.

Simbachawene amesema mawakili hao wanawajibu wa kulinda maslahi ya umma kwa kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kwamba wanatekeleza hilo kwa kutoa ushauri kwa Serikali, kusimamia kesi za Serikali na kuhakikisha kuwa shughuli zote za Serikali kujenga zinafanyika kwa msingi wa sheria.

“Mawakili wa Serikali wana nafasi kubwa katika kuimarisha utawala bora kwa kuhakikisha kuwa kuna kuwa na uwazi na uwajibikaji katika utendaji wa Serikali,”alisema.

Simbachawene amesema pia mawakili hao wananafasi kubwa ya kusaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya Madaraka na kupambana na ufisadi kwa katika kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa kikamilifu.

Aidha, Simbachawene alisema katika kuzingatia utawala bora ni lazima kuzingatia haki za watu na za Serikali na kwamba kuna wakati haki hizo zimwekuwa na msuguano (conflict).

Alitoa mfano wa mwanafalsafa wa kirusi na kimarekani ambaye aliishi kati ya 1905 hadi 1982 ambaye alisema Serikali iundwa ili kuwalinda mtu dhidi ya wahalifu huku Katiba ikiundwa kumlinda mtu dhidi ya Serikali.

Simbachawene ambaye kitaaluma pia ni mwanasheria, alisema unapoangalia mizania ya haki za watu na haki za Serikali ni lazima kuwa waangalifu.

“Sio kwamba nyie ni mawakili wa ushindi wa Serikali katika kesi. Na wakati mwingine sisi hupokea malalamiko mbalimbali kesi inaanza mahakama ya Mwanzo, mwananchi kashinda dhidi ya Serikali, Mahakama ya Wilaya mwananchi kashinda dhidi ya Serikali, Mahakama Kuu mwananchi kashinda dhidi ya Serikali,”alisema.

Alisema baada ya hapo Serikali hukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa Tanzania licha ya kushindwa katika mahakama zote hizo za chini.

“Mnapambana Serikali na mwananchi yaani hadi ngazi zote hizo bado unakata rufaa. Na maeneo mengine yanayosemwa sio maslahi ya Serikali, unakuta ni maslahi ya mtu fulani ama kikundi fulani hiyo sio sawa na huo sio utawala bora,”alisema.

Alisema kazi ya mawakili ni kulinda haki za watu au mtu lakini pia kulinda haki za Serikali.

Awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Eliezer Feleshi alisema ofisi yake inasimamia mawakili 3,486.

Alisema mafunzo hayo yanalenga katika kuwajengea uwezo mawakili wa Serikali.

“Kila tulipokuwa tukisoma taarifa mbalimbali kwa mfano ile ya Blue Print kuna maeneo mengi ambayo yanaitaka Serikali kutengeneza mazingira rafiki kwa uwekezaji,”alisema.

Alisema pia Rais Samia Suluhu Hassan aliunde Tume ya Haki Jinai ambapo kuna maeneo mengi yamependekezwa na yamekwishaamuliwa.

Alitaja mojawapo ya maeneo hayo ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Wizara ya Mambo ya Ndani kutengeneza mkakati wa kubaini na kuzuia uhalifu.

Alisema pia mawakili hao wana dhamana ya kufanya mabadiliko ya Sheria kwa kushirikiana na wadau wao.

“Kumekuwepo na mikataba, tumeona kuna mambo mapya ambayo yametusukuma (kuandaa mafunzo hayo) sio mawakili bali hata wengine kwenye Serikali walio katika shughuli za kisheria kuwa na uelewa wa pamoja,”alisema.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...