Na Jane Edward, Arusha
Naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Dkt.Franklin Rwezimula amewataka maafisa Elimu kata kuimarisha mifumo na utaratibu wa uboreshwaji wa mitaala mipya kwa kutambua kwamba ulimwengu wa sasa ni wa Sayansi,Teknolojia na Ubunifu.
Ameyasema hayo katika ufunguzi wa mafunzo ya Uanzishwaji wa madawati na majukwaa ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu yaliyofanyika jijini Arusha na kusema kuwa mafunzo hayo lengo kubwa ni kuwajengea uwezo wa kuwa wabunifu katika maeneo ya kazi kwasababu kutaongeza chachu ya mafanikio kwenye maeneo tofauti kutokana na ulimwengu huu wa sasa ni wa sayansi na Teknolojia.
"kwa ulimwengu tunaoishi huwezi kuikwepa sayansi na teknolojia ila tunachotakiwa kufanya ni kuwatambua wabunifu sehemu walipo kwa kuwafikia na kuendeleza ubunifu wao kwasababu serikali imetenga fedha kwaajili yakutekeleza ubunifu katika nyanja mbalimbali na mpaka sasa tumegundua bunifu zaidi ya 283 zilizobuniwa na watanzania huku bunifu 42 zikiwa zimeshaingia sokoni,kwa kupitia mahusiano hayo kutaongeza chachu ya ubunifu katika maeneo tofauti ya nchi yetu."alisema
Dkt.Franklin amesema kuwa washiriki wa mafunzo haya wanatakiwa kuanzisha mifumo na utaratibu wa maswala ya sayansi,teknolojia na ubunifu kwa kupanda mbegu kwa vijana ilikupata kizazi kilichobora ambacho kitapelekea nchi kuwa na wabunifu watakao kuja na bunifu zitakazokuza maendeleo ya Taifa letu.
Pia amewaasa kuwafikia vijana wengi waliopo mtaani kwa kuwekeza katika vijana hao wazawa Taifa litakuwa na wabunifu wengi, na kuwatumia vijana hao kuleta maendeleo katika nchi kuliko kutumia walioko mbali wakati ndani ya nchi tunauwezo wakutengeneza vitu wenyewe.
Naye mkurugenzi,Idara ya Sayansi,teknolojia na ubunifu (DSTI),WyEST Ladislaus Mnyone amesema mafunzo haya wizara iliandaa na kuridhia kwa uanzishwaji wa madawati ya majukwaa katika shule za msingi na sekondari ikiwa na lengo kuu la kuhakikisha kwamba wanaendelea kuimarsha utaratibu na uhamasishaji wa maswala ya sayansi na ubunifu kwasababu ni sehemu ya maisha yetu kila mahali na kwa kila ngazi hivo jamii kupata uelewa wakutosha na si tu kushiriki kama wagunduzi bali kushiriki kwa kuhakikisha kwamba wanatumia mazao hayo ya sayansi,teknolojia na ubunifu katika mizunguko ya ya maisha.
"tunahakikisha madawati yanaanzishwa katika halmashauri zote nchini na majukwaa katika shule zote za msingi,sekondari,vyuo vya ualimu pamoja na vyuo vya maendleo ya jamii iikuhakikisha kwamba kote yanapatikana madawati na majukwaa ili kuweza kuwa na wabunifu walioendelea."alisema
Pia mshiriki wa mafunzo Abubakari Hussein amesema kuwa mafunzo haya yatawasaidia na watayafanyia kazi na kwa mkoa wa Arusha watafanya vizuri kama maelekezo yalivyotolewa na kuwafikia wabunifu wa aina zote watapatikana na yale malengo ya serikali yaliyokusudiwa yatafanyiwa kazi.
Mafunzo haya yanaendelea mikoa mitatu Tanga,Dar es salaam na Arusha ikiwa lengo ni kuimarisha mfumo wa uratibu na usimamizi wa maswala ya sayansi teknolojia na ubunifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...