Na Mwandishi wetu, Manyara

WAJUMBE wa Jumuiya ya tawala za mitaa nchini, (ALAT) Mkoa wa Manyara, wametoa tamko la kumpongeza Rais wa Serikali ya awamu ya sita, Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa namna alivyoifungua Tanzania kimataifa na kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Manyara.

Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Manyara, Peter Sulle akisoma tamko hilo, amesema pamoja na Rais Samia kuifungua Tanzania kimataifa pia wanampongeza kwa kufanikisha miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali Mkoani Manyara.

Sulle amesema Rais Samia ameliunganisha Taifa la Tanzania na mataifa mbalimbali ya Afrika na dunia kwa ujumla hivyo kuwepo na ushirikiano mkubwa hivi sasa.

“Rais Samia amefanya kazi kubwa kwenye Taifa hili kwa muda mfupi wa miaka mitatu ya uongozi wake hapa nchini, kwa kuifungua Tanzania na kuwa sehemu sahihi ya utalii kwenye bara la Afrika na duniani kwa ujumla,” amesema Sulle.

Sulle amesema Rais Samia amefungua milango ya baraka kwa Taifa kwa kuipatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri za Wilaya ya Mkoa wa Manyara.

“Tunampongeza Rais Samia kwa kutuletea fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika kuboresha na kuendeleza sekta za elimu na afya katika mkoa wa Manyara,” amesema Sulle.

Amesema Rais Samia kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 kwa upande wa idara ya elimu ya msingi kwenye mkoa wa Manyara umepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 5.130.

“Kwenye bajeti hiyo halmashauri ya mji wa Mbulu imepata kiasi cha shilingi bilioni 1.2, halmashauri ya wilaya ya Mbulu shilingi 526.1 na halmashauri ya mji wa Babati ikapata shilingi milioni 363.3.” amesema Sulle.

Amesema halmashauri ya wilaya ya wilaya ya Babati ilipatiwa shilingi milioni 830.9 halmashauri ya wilaya ya Kiteto shilingi bilioni 1.221.7 halmashauri ya wilaya ya Simanjiro shilingi milioni 502.6 na halmashauri ya wilaya ya Hanang’ 474.1.

“ALAT Mkoa wa Manyara tunatoa pongezi nyingi kwa Rais Dkt Samia kwa kuwa na moyo wa upende na kuwezesha kutoa fedha hizo ambazo zitawaendeleza watoto wa Manyara na wananchi kunufaika na uongozi wake,” amesema Sulle.

Amesema kwa upande wa elimu ya sekondari kwenye mkoa wa Manyara wamepokea kiashi cha shilingi bilioni 13.912.6 ikiwa katika mgawanyo ufuatao.

Amesema halmashauri ya mji wa Mbulu imepokea shilingi bilioni 3.149 halmashauri ya wilaya ya Mbulu shilingi milioni 860.2, halmashauri ya mji wa Babati shilingi milioni 133.5, halmashauri ya Kiteto shilingi bilioni 1.368, halmashauri ya wilaya ya Babati bilioni 6.060, halmashauri ya Simanjiro shilingi bilioni 1.138 na halmashauri ya Hanang’ shilingi bilioni 1.206.

Amesema kwenye sekta ya afya halmashauri ya mji wa Mbulu imepokea shilingi milioni 950 halmashauri ya wilaya ya Mbulu shilingi bilioni 2.061, halmashauri ya mji wa Babati shilingi bilioni 2.15, halmashauri ya Kiteto shilingi milioni 989, halmashauri ya wilaya ya Babati bilioni 1.3, halmashauri ya Simanjiro shilingi bilioni 2.33 na halmashauri ya Hanang’ shilingi bilioni 1.64.

“Tunamshukuru Rais Dkt Samia kwa namna anavyowajali wana Manyara kwenye upande wa afya kwa kutupatia kiasi cha shilingi bilioni 11.425 ambazo zitaboresha maeneo mbalimbali,” amesema Sulle.

Amesema ALAT Manyara wanamshukuru Rais Dkt Samia kwani kupitia fedha hizo wana Manyara wataweza kupata huduma za afya na wataendelea kufanya kazi zao za kujiletea maendeleo na kuiamini Serikali yao ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema katika eneo la utawala halmashauri ya mji wa Mbulu imepokea shilingi bilioni 1 halmashauri ya wilaya ya Mbulu shilingi milioni 221.7, halmashauri ya mji wa Babati shilingi milioni 180, halmashauri ya Kiteto shilingi milioni 500, halmashauri ya wilaya ya Babati milioni 553.5, halmashauri ya Simanjiro shilingi bilioni 1.641 na halmashauri ya Hanang’ haikupokea fedha ila awali walipatiwa fedha nyingi ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala.

“Kwa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 mkoa wa Manyara, umepokea kiasi cha shilingi bilioni 4.046 kwenye upande wa utawala hivyo tunaendelea kumshukuru Rais Dk Samia kwani ameendelea kutupatia fedha nyingi Manyara,” amesema Sulle.

Amesema kwenye miundombinu ya barabara Mkoa wa Manyara, Rais Dkt Samia amewezesha fedha nyingi kumetolewa hivyo kufungua njia kutokana na kujengwa barabara nyingi kupitia wakala wa TARURA na TANROADS.

Amesema wanamshukuru Rais Dkt Samia kwa kuipatia Manyara fedha nyingi kwenye miradi ya maji kwani hivi anavyozungumza miradi mingi ya maji inaendelea kutekelezwa kwenye maeneo ya mkoa huo.

“ALAT Mkoa wa Manyara kwa niaba ya wananchi wa Manyara na viunga vyake tunaomba kutamka kwamba sisi wana Manyara tunamshukuru mno Rais Dkt Samia kwa upendo wake wa kutuletea maendele na kuwa tupo naye bega kwa bega na mwaka 2025 tunampa mitano tena,” amesema Sulle.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...