Dar es Salaam.Mpango wa Taifa wa Damu Salama inatarajia kukusanya chupa za damu lita 1120 katika maadhimisho ya kuelekea siku ya uchangiaji damu.

Pia imesema wana changamoto ya watu kujitokeza kuchangia damu makundi maalumu ya O,A na B Negative hivyo amewaomba watu wajitokeze wenye makundi hayo kuchangia Ili wenye huitaji huo waweze kusaidiwa

Akizungumza leo Juni 11,2024, Ofisa Uhamasishaji Damu Salama.Kanda ya Mashariki,Evelyn Dielly amesema katika kampeni ya kuelekea miaka 20 ya uchangiaji wa Damu wanatarajia kukusanya chupa lita 1120.

Dielly amesema watanzania wajitokeze kuchangia damu kwa hiari Kwa kuwa wagonjwa ni wengi wenye uhitaji wa damu hiyo.

"Leo tunajumuika na benki ya Equity katika kampeni ya kuelekea miaka 20 ya uchangiaji wa damu hivyo tunawahusisha wadai wote wajitokeze Kwa kuwa kiwanda cha kuzalisha damu ni sisi wenyewe itawasaidia wagonjwa mbalimbali wakiwemo mama mjamzito,waluopata ajali"amesema Dielly.

Dielly amesema wenye damu kundi la O,A na B Negative wanaojitokeza ni wachache hivyo amewaomba watanzania wajitokeze ili kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji wa damu wa makundi husika.

Amesema watu 100 wanaojitokeza kuchangia damu kati ya hao watano wanatoka kwenye kundi la O,A na B Negative ambao ni wachache.

Meneja Mwandamizi wa Rasilimaliwatu wa benki ya Equity, Fatma Msofe amesema benki hiyo umeamua kusaidia serikali katika uchangiaji wa damu salama.

Msofe amesema watu wamejitokeza kuchangia damu hiyo ambayo itawasidia akina mama wajawazito,watoto na wale waliopata ajali.

"Kama tunavyojua damu huwezi ukazalisha kiwandani hivyo tunawaomba watu wajitokeze katika maadhimisho ya kuelekea siku ya uchangiaji damu Ili tuweze kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji,"amesema Msofe.

Naye Abdul Nasri amesema amechangia damu kwa sababu mahitaji ya damu ni makubwa wakiwemo akina mama wajawazito na waluopata ajali.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...