Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


TUZO za makampuni bora barani Afrika (ACOYA) zilizoandaliwa na The Global CEOs Institute wakishilikiana na Eastern Star Consulting Group Tanzania zaendelea kuwa chachu ya kuongeza ufanisi na uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango ili kuleta tija katika ukuaji wa maendeleo na uchumi ndani ya Afrika.

Hayo yamesemwa Mei 31, 2024 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Group of Tanzania Bw. Deogratius John Kilawe wakati wa hafla ya kuwatunukia Tuzo Makampuni 130 yaliyofanya vizuri Barani Afrika Kwa mwaka 2024 iliyofanyika katika ukumbi wa The Superdome Masaki jijini Dar es salaam.

"Lengo ni kutambua mchango mkubwa wa Makampuni yanayofanya vizuri Barani Afrika na kuwapongeza na kuwapa moyo ili waendelee kufanya vizuri zaidi ili kuhudumia soko la Afrika Kwa huduma na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zitakazoweza kupambana na Soko la Dunia pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Afrika Kwa ujumla' Alisema.

Bw. Kilawe amesema kuwa pamoja na Mambo mengine ikiwa ni msimu wa 2 wa Tuzo hizo zilizoanza mwaka 2023 na kuleta mafanikio ya kuwaleta kwa pamoja Makampuni Makubwa zaidi Afrika na Kujadili mambo mbalimbali yatakayosaidia katika kukuza uchumi wa Afrika pamoja na kuwatunukia Tuzo Makampuni yaliyofanya vizuri zaidi.

Pia aliongeza kuwa Kwa mwaka huu ni zaidi ya nchi 20 Makampuni 700 yameshiriki katika Tuzo hizo ambapo zimepatikana Kampuni Bora 130 na kuwapatia Tuzo ili Kuchochea ufanisi na katika uzalisha wa bidhaa na huduma.

Tuzo hizo pia zimehudhuriwa na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shabani Omary pamoja na viongozi mbalimbali.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...