Na Mwandishi Wetu, Ifakara

MKUU wa mkoa wa Morogoro ,Adam Malima amekemea vikali kuwepo kwa migogoro na migongano isiyokwisha ya viongozi wa halmashauri ya mji wa Ifakara ambayo imekua ni chanzo cha kudhorotesha kwa kutokamilika miradi ya maendeleo ya huduma za kijamii na kiuchumi.


Malima amesema hayo wakati wa kikao cha Baraza maalum la Madiwani wa halmashauri ya mji huo la kupitia na kujadili hoja nane za ukaguzi zilizoibuliwa na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikli (CAG).

Amesema kuna baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo wanaendekeza majungu na migongano hata kwa kiongozi wao ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, kwa watu kushindwa kutekeleza vema majukumu yao na kusababisha halmashauri kuzidi kuzama.

" Wapo baadhi ya watendaji na wakuu wa idara mbalimbali hamtekelezi maagizo mnayopewa mkurugenzi wenu mnataka kumwamisha na tumewabaini na tutachukua hatua , mkurugenzi na wewe simamia halmashauri , kaa vyema na madiwani uwasikilize ushauri wanakupatia na mshirikiane kuketa mandeleo ya wananchi" alisisitiza Malima.


Malima amesema kuwa mivutano na migogoro hiyo imechangia zaidi ya miradi saba ya maendeleo ambayo Serikali kuu imetoa fedha nyingi kushindwa kukamilishwa kwa wakati na kuwanyima haki wananchi kunufaika na huduma za kijamii kama maji, elimu na afya kwa wakazi wa mji huo .


" .. Mimi nikiwa mkuu wa mkoa siwezi tukakaa kimya huku Ifakara inazama , watumishi na madiwani wanamagomvi …. madiwani mnamagomvi hamsimamii miradi haiwezekani.." amesema Malima .


Mkuu wa mkoa amewataja watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na madiwani kujitathimini wao kama wapo kwa maslahi yao binafsi na kama hivyo waache mara moja bali wafanye kazi kwa maslahi ya umma na kuwaletea wananchi maendeleo wanayohitaji.

" Kama wewe ni diwani nenda kajitathimini uko upande wa Diwani maendeleo au uko upande wa Diwani maslahi binafsi, kama wewe ni mtendaji kajitathimini, kama wewe ni mtendaji maendeleo au mtendaji maslahi binafsi” amesema Malima .

Mkuu wa mkoa pia aliwakata madiwani hao na watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikishwa wanaongeza nguvu katika suala la ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa matumi yake .

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara ,Kassim Nakapala ameonesha masikitiko yake ya kutokamilika kwa wakati ujenzi wa jengo la Ofisi ya za utawala wa Halmashauri uliochukua zaidi ya miaka saba na linalogharimu zaidi ya sh bilioni 7.4 ambapo ujenzi unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Licha ya kuelezea jambo hilo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kwa kuiwezesha kifedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwemo wa maji utakaowezesha kuwaondolea changamto wananchi wa Mji wa Ifakara.
Kwa upande wake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Dk Mussa Ali Musa ametumia fursa hiyo kuwataka wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa huo kupeleka Benki fedha zote za makusanyo katika Halmashauri zao kabla au ifikapo Juni 30, 2024.

Mkuu  wa mkoa wa Morogoro ,Adam Malima akisisitiza jambo kwenye   kikao cha kupitia na kujadili hoja nane za ukaguzi zilizoibuliwa na  Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikli (CAG) wakati wa Baraza maalum la Madiwani wa halmashauri ya mji Ifakara.

Mkuu  wa mkoa wa Morogoro ,Adam Malima ( kati kati) akiendesha  kikao cha kupitia na kujadili hoja nane za ukaguzi zilizoibuliwa na  Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikli (CAG) kwenye Baraza maalum la Madiwani wa halmashauri ya mji Ifakara  na (wapili kutoka kushoto) ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Dk Mussa Ali Mussa , wakati ( wakwanza kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Dustan Kyobya, wakati wapili ( kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Zahara Michuzi akifuatiwa na Mwenyekiti wa halmashauri ,Kassim Nakapala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Ifakara , Zahara Michuzi akiwa pamoja na  Mwenyekiti wake wa  halmashauri ,Kassim Nakapala ( kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo aliyeketi kulia.( Picha na Mwandishi Wetu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...