Na,Elizabeth Msagula,Lindi

Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omari amewataka watendaji kufanya ufuatiliaji na kuchukua hatua za hoja za Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuepuka kujirudia rudia na kuwa nyingi .

Ametoa rai hiyo leo Juni 25, 2024 Wilayani Nachingwea katika kikao cha baraza Maalumu la kisheria kuhusu kupitia na kujadili taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali .

''Kinachosababisha kujirudia rudia kwa hoja ni kutofanya vya kutosha na kimsingi kinachotupelekea hoja ni sisi wenyewe kuchelewa kufanya maamuzi....ni ufuatiliaji wetu tu " Zuwena Omari Katibu Tawala Lindi.

Aidha, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kupunguza hoja 7 za CAG kutoka kwenye hoja 17 na mwelekeo wa kufuta hoja 5.

Katika hatua nyingine,ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuona umuhimu wa kushiriki zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linatarajiwa kuanza siku chache zijazo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea Adinani Mpyagila amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack kwa namna anavyoendelea kuwahudumia wananchi wa mkoa huo katika kutatua changamoto mbalimbali.

" Tumeona namna ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyopambana katika kutatua changamoto za wananchi hasa kipindi kile cha mvua nyingi kilichopelekea kuaribika kwa miundombinu hasa ya barabara , amefanyakazi kubwa mnao'' Mhe. Mpyagila.

Na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea amesema Halmahauri ya Nachingwea itazingatia yote ili iendelee kufanya vizuri kwa kupata hati safi kama ambavyo imeendelea kupata miaka sita mfululizo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...