Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akishirikiana na wafanyakazi wa Taifa Gas akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Mauzo kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akizungumza na wananchi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam walipokusanyika kupata mitungi ya Taifa Gasi.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akishirikina na Kampuni ya Taifa Gesi kugawa Mitungi 300 ambayo ni sawa na milioni 22 kwa baadhi ya Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wapili wa Vyuo Vikuu jijini Dar ea Salaam pamoja na Wananchi wa Changanyikeni.

Akizungumza wakati wa Kugawa mitungi hiyo Juni 26, 2024 jijini Dar es Salaam Mtambule amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi hayana mkubwa wala mdogo ambaye hatakumbwa na mabadiliko hayo ambayo yanasaabishwa na ukataji wa miti ovyo.

Amesema kuwa hatunauwezo mkubwa wakaupamba namabadiliko ya tabia ya Nchi yanayotokea kwa sura mbalimbali hivyo tupambane na kupunguza mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutumia nishati safi ili mazingira yabaki Salama.

"Tumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha mazingira yanatunzwa, kuhakikisha mtumizi ya mkaa ambayo yamekuwa kichocheo kikubwa cha uharibifu wa mazingira tunapunguza kwa kiasi kikubwa." Amesema Mtambule.

Amesem Kampuni ya Taifa gesi inaendeleza nia njema aliyokuwa nayo Rais ya kuongeza kaya zinazotumia nishati safi kupikia.

Akizungumzia kuhusiana na afya za watu Mtambule amesema ili kupunguza mradhi na vifo vinavyotokana na nishati chafu zinazo haribu Mazingira vinatakiwa kitokomezwa kwa nguvu zote kwa kila mwananchi ili kukuza uchumi.

Amesema Matumizi ya Kuni na Mkaa yanamadhara makubwa kwasababu ukiugua matibabu yake ni gharama kubwa na inadhoofisha afya na huwezi kufanya kazi nyingine ambapo mtu akiwa mzima anafanya kazi kujiinua kiuchumi binfsi na uchumi wa taifa nzima.

"Ni mhimu kwa sasa kuongeza idadi kubwa ya wananchi wanaotumia nishati safi na salama ya kupikia."

Kwa upande wa Maneja mahusiano wa Taifa Gas, Angela Bhoke wameizungumza na Wananchi wa Changanyikeni na kutoa elimu ya hatua za kuchukua pale wanapihisi harufu ya Gesi kuvuja.

Pia ametoa elimu ya jinsi ya kujikinga na madhara yatokanayo na Moto wa gesi pale unapotokea ili kusiwe madhara makubwa ya kibinadamu.

Pia wafanyakazi hao walieleza namna ya ubebaji salama wa mitungi, usalama pale inapotokea changamoto ya kuvuja na moto.

Kwa Upande wa Wanafunzi hao, Bhoke mesema kuwa Mwanafunzi atakapo hitimi masomo yake na kwenda Nyumbani wamepewa fursa ya kurudisha mtungi na kwenda kupewa mwingine nyumbani kwao katika mikoa wanakoishi ili waendelee kutunza Mazingira kwa kutokutumia kuni na mkaa.

Kwa Upande wa mnufaika mitungi hiyo Mama Ntilie Agnes Joseph wameishukuru Kampuni ya Taifa gesi kwa msaada huo pia kwa kuwapa elimu jinsi ya kujikinga na moto uliosababishwa na gesi unapotokea.

Pia wameeleza kuwa msaada huo utaenda kuokoa mkaa na kuni zilizokuwa zikitumika wakati wa kupika chakula cha kuuza pamoja na chakula wao wenyewe.

Meneja Masoko wa Taifa Gas, Joseph Nzumbi akifafanua jambo kkwa wananchi waliokusanyika kwaajili ya kupewa mitungi ya gesi.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule akiwakabidhi mitungi kwa wanafunzi na wajasiliamali wa Changanyikeni jijini Dar es Salam.


Picha ya Pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...