Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu na kutambulisha Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, (Tax Ombudsman Services Tanzania( TOST)), uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2024.

 Msuluhishi wa Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi(TOST) Erasmus Mtui akifafanua jinsi ofisi yake inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu na kutambulisha Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, (Tax Ombudsman Services Tanzania( TOST)), uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2024.

OFISI ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, (Tax Ombudsman Services Tanzania( TOST)) leo Juni 19, 2024 wazindua kampeni ya Utoaji elimu kwa Umma ili kuitambulisha Ofisi hiyo kwa jamii.

Elimu hiyo imeshaanza kutolewa katika katika Ukumbi wa Anatoglo Mnazimmoja jijini Dar es Salaam na kuendela katika viwanja vya Mnazi mmoja na baadae katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 23 hadi 25, 2024.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewasiitiza Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na taarifa za kodi Tanzania kusimamia upatikanaji wa Vifaa na mifumo ya kisasa ili iweze kutoa huduma bora ya ulipaji kodi kwani mifumo hiyo itakusanya kodi kwaajili ya maendeleo ya taifa.

" Niwaase wafanyakazi TOST na watumishi wa TRA nchini kuhakikisha mnazingatia taratibu zote za kikodi kwa walipa kodi zinazoweza kusimamia wafanyabiashara na watu wote wanaohusika na kodi waweze kulipa kama sehemu ya kupunguza malalamiko ya kikodi.

Amesema kuwa taifa kwa sasa bado lipo kwenye mapitio ya mifumo ya kikodi ambayo hapo baadae kulingana na maoni ya wafanyabiashara inaweza kufanyiwa mapitio na mageuzi ambayo yanaweza kusaidia wafanyabiashara kuridhika na kuweza kulipa kodi kama inavyotakiwa.

Pia Chalamila amependekeza kuwepo na likizo kwa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara ambao hulipa kodi bila shuruti ili kupunguza malalamiko ya kikodi kwa Wafanyabiashara.

Pia amewaasa watanzania wote kujitokeza kutoa malalamiko na taarifa za kikodi kwani Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na taarifa za kodi( TOST) itakuwa imeanda mikakati mizuri ya usulihishi ambayo yatafikia mahala ambapo wafanyabiashara na serikali kuona kama ni ndugu na sio adui.

"TRA na Wizara ya Fedha ni chombo kinachodumisha biashara pamoja na kuandaa mazingira mazuri ya kikodi ambayo yanafundisha mfanyabiashara yeyote kuwa mwalimu na yeye kuambukiza kwa mwingine kuhusu umuhimu na umadhubuti wa ulipaji kodi." Ameeleza

Kwa upande wa Msuluhishi wa Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi(TOST) Erasmus Mtui amesema kuwa Ofisi hiyo imezindua kampeni hiyo ili kuufahamisha umma juu ya uwepo wa ofisi hiyo ili kuondoa malalamiko ya wafanyabiashara dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.

Amesema kuwa ofisi hiyo itakuwa huru katika kupokea malalamiko na taarifa za kodi zaitakazotolewa na walipa kodi au watu wenye nia njema ya kulipa kodi.

Pia Mtui amesema kuwa watakuwa wakipokea malalamiko ya Rushwa dhidi ya Watumishi wa TRA, kupokea Malalamiko ya Ukadiliaji wa kodi na uthaminishaji wa bidhaa usio n haki wala uhalisia dhidi ya TRA.

Pia watapokea malalamiko ya matumizi ya nguvu katika ukusanyaji kodi dhidi ya TRA, watapokea malalamiko dhidi ya Ufungaji biashara bila kufuata sheria dhidi ya TRA na kupokea malalamiko pamoja kero nyingine.








Baadhi ya wadau wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya utoaji elimu na kutambulisha Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, (Tax Ombudsman Services Tanzania( TOST)), uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2024.

Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...