Tume ya Madini inaendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi wote kutoka katika Mkoa wa Dodoma kwenye Wiki ya Maonesho ya Madini inayoambatana na Kongamano la Wachimbaji wa Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, leo tarehe 22 Juni 2024, Dodoma.

Elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.

Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...