Na Mwandishi wetu Dodoma

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuendelea kushirikiana na Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika mchakato wa kufanya maboresho ya mitaala ili iendane na Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala Mipya ya Elimu Msingi

Prof. Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya Tume hiyo na Vyuo Vikuu nchini kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 ambapo amewaomba Viongozi hao wa Vyuo Vikuu kutoa mrejesho pale wanapoona kuna lolote lenye changamoto ili ifanyiwe kazi katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kama unavyotarajiwa

Ameongeza kuwa majadiliano kati ya Tume hiyo na Vyuo Vikuu ni muhimu pamoja na kwamba TCU inaweza kutoa maelekezo lakini ni muhimu yafanyike kupitia majadiliano ili kuwa na ushirikishwaji wa wadau wa elimu ya juu.

"Mageuzi ya Mitaala yanagusa ngazi zote za Elimu kwa watu wanapohoji juu ya ubora wa elimu hawaangalii tu elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu bali wanagusa mpaka elimu ya juu" amesisitiza Prof. Mkenda

Kiongozi huyo ameongeza kuwa katika kutekeleza mageuzi ya elimu katika ngazi ya chini, Vyuo vikuu vinapaswa kujipanga katika kuandaa walimu wanaokwenda kufundisha katika shule za Sekondari, hivyo ni lazima kuangalia nini sera inahitaji.

Waziri huyo amesema pia katika sera na mitaala iliyoboreshwa kuna masomo mapya ambayo yanahitaji walimu akitolea mfano somo la ujasiriamali ambalo halina walimu wa kutosha na kupelekea utekelezaji wa Sera mpya katika elimu ya Sekondari kuanza na Mkondo wa Amali pekee.

Aidha, amewataka Viongozi hao wa Elimu ya Juu kuanza kujiandaa kupokea wanafunzi walisoma kidato cha tano katika mkondo wa elimu Amali ambao watakuwa na Dipmoma watakaohitaji kujiunga na shahada za amali katika fani mbalimbali.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Charles Kihampa amesema kuwa kikao hicho kitajadili juu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu na namna Vyuo Vikuu vitakavyoboresha Mitaala ili kuendana na mabadiliko haya





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...