*Mtendaji Mkuu OSHA abainisha Mipango mikakati ya utoaji huduma kwa wananchi na wawekezaji

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Serikali imesema kuwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kushirikiana na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)ili mifumo yao isomane waweze kutambua kampuni na wawekezaji ambao wamekuja nchini ili waweze kuwatambua na kuwafikia kwa wakati.

Hayo ameyasema Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira Vijana na Wenye Uemavu Deogratius Ndejembi wakati alipotembelea Banda la OSHA katika Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam pamoja na na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo ikiwemo upimaji wa Afya.

Amesema mifumo hiyo ikisomana itamsaidia OSHA kumtambua muwekezaji alipo na kumpa huduma kwa wakati na kupunguza mzunguko kwa mwekezaji

"Hii mifumo ikisomana muwekezaji akija akasajili biashara yake hapa akafungua kampuni hapa itakuwa rahisi kumfikia na kumuhudumia kwa haraka",Amesema Ndejembi

Aidha amewapongeza OSHA kwa kutumia TEHAMA kwani wamekuwa wakifanyakazi kwa ufanisi kwani taasisi hiyo ni muhimu na inatija kwa maslahi ya Taifa.

Sambamba na hayo amewataka osha kuondoa mfumo wa uaskari pindi wanapotekeleza majikumu yao badala yake watumie zaidi mazungumzo katika kuongea na waajili.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda amesema maagizo na ushauri uliotolewa na waziri watakahikisha wanaufanyia kazi kwani kwa sasa wamejipanga vizuri katika kutoa huduma kwa kuwa wamewekeza kwenye vItendea kazi vya kisasa na matumizi ya TEHAMA.

Amesema kuwa mifumo ya Tehama ndio Uwekezaji kwa OSHA na kusaidia kutoa huduma kwa wakati na tathimini zetu zinaonyesha ziko vizuri.

Mwenda amesema kuwa wana mipango mikakati ya kuhakikisha huduma zote zinapita katika mifumo iliyowekwa na anayekwamisha mfumo unasoma yote.

Amesema wameshasajili sehemu za kazi 45000 ambazo wanazipitia mara kwa mara na kuzishauri huku zoezi la kusajili likiwa linaendelea.

"Nguvu kazi iliweze kuwa na tija lazima ilindwe kwa kuonekana dhamira ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zinafikiwa" amesema Mwenda

Adha ametoa rai kwa wananchi kufika kwenye banda lao ili kupata elimu ya shughuli zao wanazofanya lakini kupata huduma ya upimaji afya bure.

"Mpaka sasa tangu sabasaba imeanza tumeshawapima afya watu zaidi ya 300 lakini pia tumekuwa sehemu ya majibu kwa maswali ambayo wadau wamekuwa wakijiuliza",Amesema.
 

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira Vijana na Wenye Uemavu Deogratius Ndejembi akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda kuhusiana utendaji wa OSHA wakati alipotembelea Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zilizo chini ya Ofisi  hiyo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira Vijana na Wenye Uemavu Deogratius Ndejembi akiteta Jambo na Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda kuhusiana utendaji wa OSHA wakati alipotembelea Banda la  OSHA kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...