Na Mwandishi Wetu.

Shule ya Msingi ya Mchepuo wa dini ya Kiislam ya Answaar iliyoko Kinondoni Studio  Jijini Dar es Salaam imeipongeza serikali kwa sera ya Elimu kwa vitendo kwani inawasadia vijana kujiajiri.

Mwalimu wa Dini dini wa Shule hiyo Ramadhani Omary Lubuva anasema kuwa serikali imeweka sera ambayo itawawezesha vijana kujiajiri na hivyo kutokaa vijiweni baada ya kumaliza masomo yao katika hatua tofauti.

“Tunaipongeza serikali kwa hatua hiyo, ni jambo jema hata hapa shuleni kwetu tunafundisha vijana ujuzi tofauti tofauti kama vile ushonaji na masomo mengine ya Dini kwa Vitendo,” anasema.

Anasema kuwa shule yao imekuwa ikiwafundisha vijana  kwa kufuata mtaala wa Wizara  ya Elimu sanjari na elimu ya Dini ya Kiislam jambo ambalo limeifanya shule kuzalisha viongozi bora kabisa wenye hofu ya Mungu.

“Tuna wakuu wa Wilaya , Wataalam mbalimbali wa serikali waliopitia shuleni hapa na kwamba huko waliko wamekuwa viongozi bora sana kwani wana maadili pia wana hofu ya Mungu,” anasema.

Anafafanua kuwa wanafundisha vijana wa madhehebu mbalimbali kama vile Wakrito na wasio na dini hapa, wanaletwa na wazazi wao kwa lengo la kupata elimu yenye maadili mema,” anasema .

Anafafanua kuwa siyo rahisi kwa vijana wanaopita shuleni hapo kuwa wala rushwa au mafisadi kwani wanajifunza elimu ambayo inawapa hofu ya Mungu.Anatoa wito kwa wananchi kupeleka watoto shuleni hapo 

Mwalimu wa Dini wa Shule Kiislam Ramadhan Omary Lubu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...