Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (kulia) na Prof. Detflef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn (kushoto) wakitia Saini ya Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn

**********************

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema Mzumbe iko tayari kushirikiana na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi katika kubadilishana uzoefu katika maeneo ya taaluma na tafiti.

Prof. Mwegoha amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn yanalolenga kuimarisha uhusiano wa kitaaluma na kuboresha ubora wa elimu, utafiti na ubunifu baina ya vyuo hivyo.

Awali, Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn amesema ni fursa kwao kuimarisha ushirikiano utakaoleta tija baina vyuo hivyo kwa kuinua viwango vya elimu ya juu na utafiti katika nyanja mbalimbali huku ukihimiza uvumbuzi na ubunifu.

Makubaliano hayo ya ushirikiano yanaelekeza ushiriki wa Chuo Kikuu Mzumbe katika miradi ya utafiti na kuboresha mitaala ili kukidhi mahitaji ya soko ya ajira kimataifa. Pia, ushirikiano huo utaleta fursa za semina, warsha na kongamano za kitaaluma zinazolenga kujadili changamoto na mbinu bora za kuboresha elimu na utafiti.

Hati ya makubaliano baina ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo cha Bonn ni ya miaka mitano kufuatia kukamilika kwa awamu ya kwanza ambapo wanataaluma wamenufaika na fursa za masomo na tafiti katika nyanja za taaluma na tafiti.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn kwenye Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn
Prof. Detlef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (kulia) akikabidhi zawadi ya kumbukumbu kwa Prof. Detflef Mueller-Mahn kutoka Chuo Kikuu cha Bonn (kushoto) baada ya Hafla ya Utiaji Saini wa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn
Chuo Kikuu Mzumbe na Chuo Kikuu cha Bonn vyasaini Hati ya Makubaliano katika kuimarisha taaluma na tafiti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...