Katika jitihada kubwa za kuboresha elimu ya wasichana na kuongeza uelewa kuhusu hedhi salama, Kampuni ya Sukari Kilombero imetoa zaidi ya taulo za kike 2,400 kwa wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Cane Growers iliyopo wilayani Kilombero.
Jitihada hii inaonyesha ahadi ya Kampuni hiyo katika kukabiliana na tatizo la hedhi salama na kusaidia jamii inazo hudumia.
Kupitia hafla ya kukabidhi msaada huo ambayo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Cane Growers, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Ndugu Abraham Mwaikwila, aliipongeza Kampuni ya Sukari Kilombero kwa jitihada zake katika kusaidia elimu ya wasichana. Alisema, "Mchango huu kutoka Kampuni ya Sukari Kilombero ni zaidi ya msaada bali ni ishara kubwa ya kuunga mkono wasichana hawa wanaosoma ndani ya wilaya yetu.
Kwa kutoa taulo hizi za kike, Kilombero Sugar inasaidia kuondoa kikwazo kikubwa kwa elimu. Jitihada hii siyo tu inawasaidia wasichana kubaki shuleni bali pia inawawezesha kuwa na ujasiri wa kufuata ndoto zao bila shida yoyote. Tunashukuru sana kwa mchango huu wenye msaada mkubwa kwa mustakabali wa jamii yetu."
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kilombero Sugar, Bi. Diana Mwakitange, alisema kuwa Kampuni ya Sukari Kilombero leo inakabidhi taulo za kike 2,400 kwa shule kama sehemu ya ahadi yetu ya kibiashara ya kuimarisha jamii tunayoihudumia. Bi. Mwakitange aliongeza kuwa anafurahi kwamba asilimia 65 ya wanafunzi katika shule hii ni wasichana, akisisitiza lengo la kuwahifadhi wasichana shuleni kwa kupambana na tatizo la hedhi salama. Pia alibainisha kuwa jitihada hii inaendana na ajenda ya kitaifa ya kuboresha elimu ya wasichana na kupunguza tofauti za kijinsia shuleni. "Kwa kuhakikisha kuwa wasichana wanapata taulo za kike, tunachangia moja kwa moja katika mafanikio yao ya kitaaluma na ustawi wao."
Kwa upande wake, Meneja wa Mawasiliano na Mahusiano ya Wadau wa Kampuni ya Sukari Kilombero, Bw. Victor Byemelwa, alisisitiza dhamira ya Kampuni hiyo ya kuhakikisha hakuna msichana anayekosa shule kwa sababu ya mzunguko wake wa hedhi. "Tunatambua changamoto ambazo wasichana wengi wanakutana nazo katika kusimamia hedhi salama hasa katika jamii ambazo hazihudumiwi ipasavyo. Kupitia shughuli zetu za kurudisha kwa jamii kama hii, tunalenga kuwawezesha wasichana hawa kwa kuwapatia rasilimali muhimu za kusimamia hedhi salama. Kwetu hii siyo tu kutoa msaada wa taulo za kike, bali kuunda mazingira ambapo suala la hedhi salama linakuwa ni la kawaida bila unyanyapaa," alisema Bw. Byemelwa.
Kampuni ya Sukari Kilombero inaendelea kuonyesha dhamira yake ya uwajibikaji wa kijamii kupitia mipango inayoelekezwa kwenye elimu, afya, na maendeleo ya jamii kote Tanzania.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero, Bw. Abraham Mwaikwila (wa pili kushoto), akiungana na Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Kampuni ya Sukari Kilombero Bi. Diana Mwakitange (wa tatu kulia), kukabidhi taulo za kike 2,400 kwa Shule ya Sekondari ya Cane Growers iliyopo wilayani Kilombero leo. Mpango huu unaonesha dhamira ya kampuni hiyo katika kupambana na changamoto za hedhi salama na kusaidia jamii ambazo wanafanya kazi. Wengine katika picha ni: - Meneja Mawasiliano na Uhusiano na Wadau, Bw. Victor Byemelwa (wa pili kulia), Meneja wa Masuala ya Biashara, Willa Haonga (kulia) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Cane Growers, Bw. Yusufu Lauwo (kushoto).
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Cane Growers wakionyesha maboksi ya pedi za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kilombero Sugar leo wilayani Kilombero. Mchango huu, ambao ni sehemu ya mpango wa 'Kukomesha changamoto ya hedhi salama, unaonyesha dhamira ya kampuni hiyo katika kuendelea kupambana na changamoto hiyo na kusaidia jamii wanazo zihudumia.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...