Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya ameelezea kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Itembe mkoani Simiyu na kusisitiza likamilike kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 150 liko katika barabara ya Maswa-Meatu-Sibiti hadi Karatu inayounganisha kwa njia fupi mikoa ya Kanda ya ziwa na Kaskazini ambapo kukamilika kwake kutaleta tija kwa sekta ya usafirishaji, uzalishaji na utalii kwa wakazi wa mikoa hiyo.

" Kazi yenu ni nzuri mko asilimia 80 hakikisheni kasi yenu inaendana na ubora ili Serikali izidi kuwaamini na kuwapa miradi mingi wakandarasi wazawa", amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS),Mkoa wa Simiyu Eng. Boniface Mkumbo amesema daraja hilo linalojengwa na mkandarasi mzawa Roctronic Ltd pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa KM 2 litagharimu zaidi ya shilingi bilioni 9.4 litakapokamilika.

Amesema katika kuhakikisha barabara hiyo ya inaimarika na kupitika wakati wote wa mwaka maandalizi ya kujenga madaraja ya Chobe mita 100 na Lyusa mita 75 yako katika hatua za mwisho.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...