Meneja Uhusiano wa kampuni ya MICO International Halal Bureau Limited, Mohamed Matano, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la Halal litakalofanyika siku ya Jumatano katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya MICO International Halal Bureau Limited, imeandaa kongamano la kimataifa la wadau wa Hahal litakalofanyika siku ya Jumatano Agosti 14,2024 jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Mohamed Matano, amesema MICO ni kampuni pekee Tanzania ambayo inatoa ithibati ya Halal kwa wafanyabiashara na kampuni zinazotoa huduma ndani ya nchi.

Amesema kampuni ya MICO ndiyo inatoa ithibati kwa kampuni zote zinazofanya uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma mbalimbali hapa nchini.

“Tarehe 14 mwezi wa nane kutakuwa na kongamano la pili la kimataifa katika ukumbi wa kimataifaa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na tunatanarajia kukutana na wadau wa Halal hapa nchini,” amesema.

“Tanzania tunanafasi kubwa ya kufanya Halal Industries katika utalii, katika dawa, famasia na fedha kwa hiyo tutakapokutana na wadau tutajadiliana namna ya kuboresha shughuli za Halal hapa nchini,” amesema

Amesema wadau mbalimbali na viongozi wa serikali watahudhuria kongamano hilo la wadau wa Halali ambalo linakadiriwa kushirikisha washiriki 500 wanaofanya kazi kwenye kampuni mbalimbali.

“Kutakuwa na muda wa B2B yaani mtu mmoja mmoja kukaa na kuzungumzia masuala mbalimbali ya Halal kwa hiyo tunaomba wananchi wote wanaopenda kushiriki kongamano hili wajisajili,” ameongeza kusema

Amesema MICO International Halal ndiyo inasimamia machinjio yote Tanzania kwa kuwafundisha wachinjaji mafunzo ya Halal na kuhakikisha machinjio hayo yanaendeshwa katika misingi ya Halal.

Amesema kampuni hiyo ilipewa idhini ya kuendesha shughuli hiyo na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...