Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameielekeza Wizara ya Ujenzi kuharakisha mchakato wa kumpata Mkandarasi mpya atakayejenga Barabara ya kutoka Sengerema hadi Nyehunge, jimboni Bushosa yenye urefu wa Kilometa 54.5, ili kazi ya ujenzi ianze mapema.

Aidha ameitaka Wizara hiyo, kuimarisha mchakato wa kukagua Wakandarasi ili wapatikane Wakandarasi wenye uwezo.

Balozi Dokta Nchimbi amesema hayo Agosti 13, 2024, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Nyehunge Jimboni Buchosa wilayani Sengerema,mara baada ya kuwasili Jijini Mwanza kuanza ziara yake ya siku 2 mkoani humo.

Balozi Nchimbi ameelekeza mchakato ufanyike haraka ili Mkandarasi apatikane na kazi ianze ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami.

Kuhusu kuimarisha uwezo wa kubaini Wakandarasi wenye uwezo, Balozi Dokta Nchimbi amesema hiyo itasaidia kwani wako Wakandarasi ambao wana historia ya kuharibu kila sehemu,na wanakimbilia Tanzania.

Amesema kamwe watu wasipewe kazi kwa majaribio.

Awali Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema Mkandarasi huyo wa kituruki pia alipewa kazi Kyela mkoani Mbeya ambako ndiko alikoanza,lakini akaanza kusuasua.

Mhandisi Kasekenya amesema baada ya kuona Mkandarasi huyo anasuasua Kyela,Serikali ilifuatilia na ikaona uwezo wake ni mdogo.

Amesema kutokana na kubaini hilo,Serikali iliamua kusitisha Mkataba licha ya kwamba alikua ameshakabidhiwa hiyo Barabara.

Amesema Serikali ilitambua uwezo wa Mkandarasi huyo ni mdogo na amefafanua kwa sasa Serikali inakamilisha taratibu za kuvunja huo Mkataba ambao ni mkataba wa kimataifa.

Mhandisi Kasekenya amesema baada ya hapo,Serikali itatafuta Mkandarasi mwingine na kusema kama sheria itaruhusu, aliyekua wa pili apewe Kandarasi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...