Serikali imesema ipo katika mipango ya kuboresha mifumo ya utoaji huduma sekta binafsi ikiwemo kutengeneza mazingira rafiki katika nyanja mbalimbali jambo ambalo lisaidia kuongeza tija kwa kuongeza mapato kupitia kodi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Agosti 7, 2024 akiwa katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari Kavu ya Bravo, AGL na Kampuni ya CMA-CGM, Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile, ameipongeza jitihada zinazofanywa na kampuni hizo ikiwemo kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga uchumi wa Taifa.

Mhe. Kihenzile amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo Bandari, Meli, Reli pamoja na Viwanja vya ndege.

“Wanafanya kazi kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kulipa kodi ambayo inatumika kujenga miundombinu ya barabara, kutoa huduma ya maji, umeme pamoja na kupunguza msongamano wa mizigo bandarini” amesema Mhe. Kihenzile.

Mhe. Kihenzile amesema kuwa wanakwenda kulifanyia kazi ombi la sekta binafsi kuhusu madai yao ya kutaka serikali kufikilia namna ya kuongeza muda wa leseni zao kutoka mwaka mmoja hadi miaka mitano kutokana wanashindwa kuandaa vizuri mipango yao ya biashara ya muda mrefu kwa ajili kuomba mkopo katika taasisi za fedha.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali, amesema kuwa usafirishaji kwa njia ya maji kuna wadau wengi ikiwemo bandari kavu, hivyo wamekuja kuona utendaji kazi wao baada ya kupewa majukumu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

“Tumekuja kuona wamejipangeje kutoa mchango wa kuendeleza uchumi wa Taifa, tumeona mambo mengi mazuri wanayofanya, pia tumesikiliza changamoto zao na zinakwenda kutatuliwa” Bw. Mlali.

Amesema kuwa TASAC wana jukumu la kuwapa leseni wanaofanya biashara hizo na wamekuwa na utamaduni wa kuwatembelea mara kwa mara kwa ajili ya kuwakagua ili kuona wanatekeleza masharti ya leseni zao.

Nao AGL Logistics pamoja na Bravo Logistics wamefurahia ujio wa Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile ambapo wamepata fursa ya kueleza changamoto zao katika kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kuchangia katika pato la Taifa.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiwa kwenye ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Bravo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali katika ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu ya Bravo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea na kukagua Bandari kavu ya Bravo ili kusikiliza changamoto wanazopitia ili kuweza kuja na majibu sahihi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na uongozi wa uongozi wa Bandari kavu ya AGL iliyopo Mwananchi jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali alipokuwa anaeleza kuhusu namna wanavyoisimia Bandari kavu ya AGL ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiwa kwenye ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za Bandari kavu yaAGL iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akizungumza na uongozi wa uongozi wa Kampuni ya CMA-CGM alipofanya ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za katika Kampuni hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya CMA-CGM wakifuatilia mazungumzo ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile alipofanya ziara ya kukagua na kusikiliza changamoto za katika Kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw. Nelson Mlali pamoja na uongozi wa Kampuni ya Uwakala wa Meli ya CMA-CGM mara baada ya kumaliza kuzungumza na uongozi wa Kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...