Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza katika Kongamano la Uwekezaji katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza kuhusiana Uwekezaji wa miradi ya Serikali ya kuvutia wawekezaji, kwenye Kongamano la Uwekezaji lililofanyika katika Maonesho ya Kilimo Kitaifa Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.



Baadhi ya Washiriki katika Kongamano la Uwekezaji.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema suala la Uwekezaji nchini ni jambo mhimu katika kuondokana na umasikini.

Serikali inataka watumishi wote wa umma waliokabidhiwa dhamana katika utumishi watambue wanajukumu la msingi la kukuza biashara na kuzitafutia soko hiyo ndio kazi yetu.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 6 2024 wakati akifungua Kongamano la uwekezaji katika sekta za utalii, kilimo lilofanyika kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Profesa Mkumbo amesema kuwa mpango wao wa maendeleo wa mwaka 2024/2025 wana maeneo kumi yaliyopewa msukumo na baadhi ya maeneo hayo ni pamoja kuendelea kuwekeza katika kukuza uzalishaji katika sekta ya kilimo.

"Kuendelea kuhamasisha na kuwezesha matumizi ya mbegu bora, matumizi ya mbolea, kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya zana za kisasa katika kilimo. Kama tunavyofahamu, uchumi wa viwanda tunaojaribu kuujenga malighafi zake nyingi asilimia 65 zinategemea kilimo," amesema

Aidha Profesa Mkumbo amesema kipindi cha muda mfupi na muda wa kati, watanzania wengi wataendelea kuajiriwa na kujiajiri katika sekta ya kilimo.

Akizungumzia kuhusu Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Profesa Mkumbo amesema mujibu wa takwimu za TIC sekta tano zinavutia zaidi uwekezaji nchini ni uzalishaji viwandani, usafiri na usafirishaji, ujenzi wa majengo ya biashara, utalii na kilimo.

Profesa Mkumbo kwa kuzingatia idadi ya miradi inayosajiliwa na TIC (2021-2024), kati ya miradi 1484 iliyosajiliwa katika kipindi hiki, uzalishaji viwandani unaongoza 608 Sawa na asilimia 41, ukifuatiwa na usafiri na usafirishaji 262, Sawa na asilimia 17.6, utalii 142 sea na asilimia 9.5 majengo ya biashara 140 Sawa na asilimia 9.4, na kilimo 123, sawa na asilimia 8.

Hata hivyo, kwa kuzingatia idadi ya ajira zinazozalishwa na miradi ya uwekezaji kilimo kinaongezeka.

Amesema kati ya ajira 353,133 zilizotarajiwa kuzalishwa kutokana na miradi ya uwekezaji katika kipindi tajwa jumla ya ajira 115,212 sawa na asilimia 32.7 zilitokana na kilimo, ikifuatiwa na viwanda 95,397 Sawa na asilimia 27 usafiri na usafirishaji 39,230 Sawa na asilimia 11.1, majengo ya biashara 11,212 Sawa na asilimia 3.2 na utalii 10,266 Sawa na asilimia 2.9.

Amesema Wakuu wa wilaya,Mikoa na wakurugenzi wanapaswa kushindana kwa idadi ya biashara na uwekezaji waliosababisha kutokea na kukua katika maeneo yao ya kazi.

Amesema sekta ya kilimo ni chanzo kikubwa cha ajira, kwa vijana,ambapo kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa nguvu kazi nchini ya mwaka 2020/2021 ni asilimia 54.8 ya idadi ya watu wote nchini. Hii ni sawa na watu milioni 34. Kati ya idadi hii, watu milioni 28.6

Amesema kila mwaka, Agasti 8 nchi huadhimisha siku ya wakulima kwa kutambua mchango wao mkubwa katika uhai wa Taifa letu na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

"Sekta ya kilimo katika maisha na maendeleo ya nchi yetu ni dhahiri. Kwanza, kilimo ndicho kinachotupa chakula, ambayo ni hatua ya kwanza katika maisha ya binadamu.

Hata hivyo amesema jambo la Pili, sekta ya kilimo inachangia asilimia 26 ya pato la taifa. Hii inamaanisha kuwa katika pato la taifa la shilingi trilioni 148.7 trilioni 38 zinatokana na sekta za kilimo.

Amesema wanaojishughulisha kikamilifu na shughuli za kiuchumi ambapo asilimia 65 wanajishughulisha na shughuli katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji,"amesema.

Amefafanua sehemu ya pili ni kuchochea na kuvutia uwekezaji katika viwanda vyenye kulenga kuzalisha bidhaa zitakazoifanya nchi jitosheleze kwa mahitaji ya bidhaa muhimu nchini na kukuza mauzo ya bidhaa zilizoongezwa thamani nje ya nchi.

"Tunaagiza kutoka nje ya nchi Bidhaa hizi ni pamoja na mafuta ya kula, sukari, ngano na mazao mengine.

Amesema mauzo ya nje ya nchi bado yametawaliwa kwa kiasi kikubwa na bidhaa ambazo hazijaongezwa thamani hivyo kunahitajika kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuchochea ukuaji wa sekta binafsi, hususan tukilenga kuweka mazingira maalum ya kukuza na kuimarisha biashara na uwekezaji katika sekta ya biashara ndogo na ya kati.

Nae Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda amesema kwenye kongamano hilo wawasikilize wataalamu nini kifanyike katika kuendeleza kilimo na uzalishaji bora wa mazao.

"Niwapongeze mlioandaa kongamano hili kwaajili ya kutoa utalaamu kutoka kwa wataalamu mbalimbali japo bado kuna tatizo hatujui jinsi gani ya kutumia fursa," amesema Pinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...