Benki ya Tanzania (TCB) inayo furaha kumkaribisha Bi Lilian Mtali kuwa Mkurugenzi wa Biashara za wateja Wadogo na wa Kati. Bi. Mtali ana uzoefu wa miaka 26 katika sekta ya huduma ya kifedha akibobea katika usimamizi na uongozi wa huduma za biashara za wateja wateja wadogo, wa kati na wakubwa.

Bi. Mtali amefanya kazi na kupata uzoefu wa uongozi kutoka benki mbalimbali za hapa nchini na za kimataifa, amefanya kazi katika benki za I&M Bank Tanzania Limited,  Standard Chartered, Stanbic na DCB akishika nyadhifa mbalimbali za uongozi kama Meneja wa tawi, Mshauri wa Masuala ya Fedha (Personal Financial Consultant, Meneja Uhusiano wa Wateja (Priority banking) Meneja wa Huduma kwa Wateja na Ubora wa Huduma na Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Wadogo na Wakubwa.


Katika utendaji wake, Bi. Mtali amefanya mabadiliko makubwa katika ukuaji na maendeleo ya taasisi zote alizofanya kazi,Amesimamia miradi mbalimbali ya kibenki kwa ujumla ikiwemo kuongeza wigo wa mikopo ya biashara kwa wateja wadogo, kusimamia ukuaji wa wateja binafsi (High Valued Customers), kusimamia ukuaji wa huduma za uwakala usimamizi, na mikopo ya kidigitali.


Bi.  Mtali amekuwa nguzo ya uongozi, katika kuleta mabadiliko chanya ya taasisi na kuchochea mabadiliko ya uendeshaji biashara na utendaji wa taasisi.


Bi. Mtali ana Shahada ya Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo cha Kimataifa cha Amerika (IUA), London Campus, United Kingdom na Cheti kutoka Modern Tutorial College, London, United Kingdom. Aidha, amesoma kozi na semina mbalimbali za uongozi wa kimataifa kutoka United Kingdom, Afrika Kusini, Kenya, Zimbabwe, Angola na Singapore.


Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Bwana Adam Mihayo akiongea kuhusu ujio wa Bi. Lilian Mtali katika Benki ya TCB alisema ana imani na uzoefu mkubwa wa Bi. Mtali pamoja na uwezo wake wa uongozi hivyo ni matumaini yao kwamba atakuwa msaada mkubwa wakati huu tunapoendelea kuboresha huduma za wateja wa rejareja, wadogo na wa kati.


Taarifa hii imetolewa na kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Tanzania Commercial Bank (TCB)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...