Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Dodoma
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imesema kuwa baadhi ya kodi katika sekta ya Kilimo ikiwa na lengo la kuchochea Kilimo na kutaka wakulima kutoa ushirikiano wa kulipa kodi.
Hayo ameyasema Afisa msimamizi wa kodi wa TRA Philip Eliamini wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Banda la TRA katika Maonesho ya Kilimo na Ufugaji Nane Nane inayofanyika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema wakulima na wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao ili kupata elimu ya kodi lakini pia kufahamu bidhaa za kilimo zilizo kwenye msamaha wa kodi.
Amesema wamejikita kutoa elimu ya kodi kwenye maonesho hayo kwani wakulima ni wadau wazuri wa kodi na serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuwainua wakulima kuweza kufanya Kilimo Biashara na kuweza kulipa kodi.
"Nawasihi wakulima wafike kwenye viwanja kupata faida na kujifunza masuala ya msingi ya kodi katika kilimo".amesema Eliamini
Amesema kujifunza masuala ya kodi kunasaidia kuepukana na taarifa sisizo sahihi.
Sambamba na hayo Eliamin amesema pia wanatoa huduma ya namba ya mlipa kodi (TIN NAMBA) kwa watu ambao awana lakini wanatoa huduma ya ukadiliaji kodi kwa wafanyabiashara.
Aidha amesema kila mfanyabiashara mwenye mauzo ya milioni 11 kwa mwaka anapaswa kutumia mashine ya EFD na kusaidia Serikali kupata mapato na kwenda kuhudumia wananchi.
Aidha ameongeza kuwa maagizo yaliyotolewa na katibu mkuu wizara Uvuvi na Mifugo Profesa Shemdoe watayafanyia kazi na amewataka wadau pia kuyafanyia kazi kwani amewataka wadau wanaoagiza bidhaa zilizo kwenye msamaha kodi kuwasilisha nyaraka zao kwa TRA mapema kabla ya bidhaa hizo kufika lakini pia amewataka watendaji wa TRA kufanyakazi kwa bidii na weledi.
Afisa Mwandamizi wa TRA Philip Eliamini akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya Nane Nane Dodoma kuhusiana na wakulima kupata elimu ya Kodi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...