Na. Ramadhani Kissimba, WF, Morogoro


Watoa huduma ndogo za fedha  na vikundi vya kijamii nchini  vinavyojihusisha na huduma za mikopo vimetakiwa kuwapatia nakala ya mkataba wananchi wanaowakopesha mikopo.
 
Akizungumza katika program ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Mji Mdogo wa Mikumi, Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha Bi. Grace Muiyanza, alisema kuwa watoa huduma wanatakiwa kutoa mikataba kwa wanaowakopesha kwa mujibu wa sheria iliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania.
 
Aidha Bi Muiyanza alisema mkataba ni mafungamano kati ya pande mbili ya mkopeshaji na mkopaji hivyo ni lazima kila upande uridhie makubaliano hayo kabla ya kuchukua mkopo na kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kurejesha mkopo na pia mkataba utakuwa ndio njia pekee ya kila mmoja kupata haki yake itakapotokea mgongano baina yao.
 
Pia, Bi. Muiyaza aliwasihi wananchi kabla ya kusaini mkataba wa mkopo ni vizuri kila mmoja akapata nafasi ya kuusoma na kuelewa masharti ya mkataba huo ili usije ukamfunga kwa vipengele ambavyo vitasababisha ugumu wa kurejesha mkopo wake.
 
‘’Mkataba ni masharti ya pande mbili, hakikisha umeusoma na kuuelewa mkataba, na hata kama ujui kusoma nenda kwa maafisa wa maendeleo ya jamii wakueleweshe masharti yaliyomo kwenye mkataba huo maana ukiamua kusaini bila ya kuuelewa utakuwa umeshakubaliana na masharti na utakuwa umesaini masharti yatakayokuja kukufunga baadae’’. Alisema Bi Muiyaza
 
Awali akifungua mafunzo hayo Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mikumi Bi. Edith Mlay, aliwataka wananchi wa Mikumi kuitumia fursa hiyo ya kujifunza masuala ya fedha ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kutoka kwa baadhi ya watoa huduma za fedha. 
 
Bi. Mlay aliongeza kuwa elimu ya fedha ni muhimu sana kwa wananchi wa Mikumi kwa sababu mji huo umekusanya makundi muhimu ya kijamii yakiwemo ya wakulima na wafugaji, hivyo elimu hiyo itawasaidia wananchi hao kutumia fursa ya uwekezaji zilizopo katika sekta ya fedha baada ya kuuza mazao yao.
 
Wizara ya Fedha na washirika wa sekta ya fedha nchini imehitimisha program maalum ya elimu ya fedha kwa umma kwa Mkoa wa Morogoro ambapo elimu hiyo ilitolewa katika Halmashauri saba (7) ambazo ni Halmashauri ya Morogoro Mjini, Morogoro vijijini, Kilosa, Mvomero, Ifakara, Mlimba na Gairo.
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyaza, akiongea na wananchi wa Mikese Mkoani Morogoro katika program ya elimu ya fedha yaliyotolewa kwa wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo Mikumi.

Afisa Masoko Mwandamizi kutoka Kampuni ya Uwekezaji ya UTT Bw. Rahim Mwanga akiongea na washiriki wa program ya elimu ya fedha kwa umma (hawapo pichani) iliyotolewa katika Mji mdogo wa Mikumi Mkoani Morogoro.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Grace Muiyaza, akiongea katika kikao kati ya timu ya wataalamu wa masuala ya fedha na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa (hayupo pichani) walipotembelea ofisini hapo kabla ya kuanza kwa program ya elimu ya fedha kwa wananchi wa Kilosa. Pembeni kwa Bi. Grace ni Afisa Mipango kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko na Dhamana Bw.Godfrey Makoi na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Jackson Mushumba.

Wananchi wa Mji Mdogo wa Mikumi wakimsikiliza mtaalamu kutoka Kampuni ya Uwekezaji ya UTT (UTT-AMIS) Bw. Rahim Mwanga, wakati wa program ya elimu ya fedha kwa umma iliyotolewa kwa wananchi hao.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha – Morogoro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...