Na Mwandishi Wetu , Michuzi TV Ukerewe

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo tarehe 10.9.2024, limetoa elimu ya ulinzi, usalama na utunzaji wa mzingira ya usafiri majini kwa wadau mbalimbali wa usafiri majini katika Kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe.

 Elimu hiyo imehusisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wasafiri na wasafirishaji, wamiliki wa vyombo vya usafiri majini, viongozi wa serikali za Kijiji na wananchi kwa ujumla. 

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika mwalo wa Bukungu Naho. Michael Rogers amesema ”kila mmoja ni balozi wa usalama wa vyombo vya usafiri majini hivyo hatuna budi kuhakikisha vyombo vinakidhi viwango na kuhakikisha vinakuwa na leseni kwa mujibu wa sheria na kupunguza ajali za mara kwa mara kwa kuvaa vifaa vya kujiokolea kwani kila mmoja wetu ni muhimu kwa jamii na taifa kwa ujumla”

Aidha, wananchi wa Ukerewe katika mialo iliyotembelewa na TASAC wamepongeza na kushukuru juhudi za utoaji elimu na kuomba Shirika kuendelea kufanya hivo mara kwa mara ili kuongeza uelewa mpana kwa wananchi juu ya sekta ya usafiri majini.

Zoezi hili la utoaji elimu limeanza Septemba 9 na litafikia tamati Septemba 13,2024.
Afisa Mfawidhi, Ofisi ya TASAC Wilaya ya Ukerewe Michael Rogers akizungumza katika mkutano wa kutoa elimu ya ulinzi, usalama na utunzaji wa mzingira ya usafiri majini uliofanyika   katika Mwalo wa Bukungu Naho Ukerewe mkoani Mwanza.
Mratibu na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii na Mahusiano ASP. Wilaya ya Ukerewe Raphael Ganchira akizungumza katika utoaji wa elimu wa wadau  wa usafiri wa majini katika Mwalo wa Bukungu Naho Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
 Baadhi ya wananchi wakipata elimu ya Usalama,Ulinzi na Utuzaji wa Mazingira katika Mwalo wa Bukungu Naho wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.


Baadhi ya wananchi wakipata elimu ya Usalama,Ulinzi na Utuzaji wa Mazingira katika Mwalo wa Bukungu Naho wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...