Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya waendesha baiskeli kuelekea Butiama 2024, ambayo inadhaminiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic.

 Uzinduzi huu ulifanyika kama maendesho ya baiskeli ya kijamii "Pedal for Purpose," ambayo ni mwanzo wa ziara hii kuelekea Butiama. 

Benki ya Stanbic imechangia kiasi cha shilingi milioni 70, ambazo zitatumika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa madawati 1,500, sekta ya afya kwa kuanzisha kliniki zinazozunguka kuhudumia mikoa mbalimbali, na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 50,000. 

Kiujumla ziara hii inategemea kuboresha Maisha ya watanzania 100,000. Kilele cha ziara hiyo kitafanyika Butiama, mkoani Mara, tarehe 14 Oktoba.

Mchezaji wa zamani toka Nigeria, Nwankwo Kanu (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi  Vodacom Twende Butiama 2024 uliofanyika jijini Dar es salaam. 








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...