*Dk.Nchimbi asema Chama kimesikitishwa, uchunguzi ufanyike
*Awaomba viongozi vyama vya upinzani kushirikiana badala ya kufarakana
*Agusia kauli za kuligombanisha Jeshi la Polisi na wananchi
*Asema waliotekwa mpaka sasa ni watu 152, waliopatikana 141
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kimesikitishwa na tukio la mauaji ambalo limefanywa kwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Ali Kibao na kusisitiza wanaungana na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan uchunguzi ufanyike haraka na watakaobainika sheria ichukue mkondo wake.
Pia Chama kimesema kinataka kuona waliohusika wanapatikana kwa gharama yoyote na iwapo Serikali itaona kuna ulazima wa kuwa na wachunguzi kutoka nje ya nchi Chama hicho kitaunga mkono kwani wanachotaka ni kuona wahusika wanapatikana kwa gharama yoyote.
Akizungumza leo Septemba 13,2023 jijini Dar es Salaam na Wahariri na waandishi wa habari nchini ,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi amesema Chama hicho kinasikitishwa na tukio la mauaji ya Ali Kibao na kusisitiza kinalaani tukio hilo.
“Kama mnavyofahamu siku chache zilizopita ndugu Ali Mohamed Kibao alitekwa na watu wengi wamezungumza.Chama inataka kulisemea kidogo historia nzuri ya nchi yetu tangu tupate uhuru.
“Tumeendelea kujenga umoja na kuwa nchi ya mfano, misingi muhimu ambayo imewekwa na kujenga umoja na mshikamano ni pamoja na utu, katika miaka 60 tumepita nyakati nzuri kama taifa na tumepita nyakati mbaya lakini bado tumeendelea kuwa na mshikamano,”amesema Dk.Nchimbi.
Akiendelea kueleza Dk.Nchimbi amesema leo nchi inapita katika changamoto nyingine ambayo imezua hofu.Ilani ya CCM kipengele cha 105k moja ya mambo wanayofanya ni kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi zao.
“Suala la amani, tulivu, usalama wa rai ana mali za oni moja ya mambo muhimu ambayo CCM inataka kuona yanatekelezwa kikamilifu.Mtu yoyote anayeteka mtu anayeshiriki katika mauji ya raia, ama kikundi chochote kinachofanya hivyo kinajua kinafanya ili kuijengea CCM nia mbaya…
“Na mtu yoyote anayefanya hivyo anajua anaimuza CCM .Lakini lazima niseme CCM sio ya watu wajinga, haijiwezi kujimaliza chenyewe, ni chama cha siasa kisichojitambua ambacho kinaweza kufanya matukio ya hovyo…
“Ndio maana tunapita kila siku kueleze utekelezaji wa Ilani lakini nia kubwa kuliko zote ni kuwafanya wananchi wawe na imani.Watu wenye nia mbaya ndio wanaofarakanisha taifa na Chama, ndio watu hawa hawa wanasababisha watu wenye busara waongee mambo yasiyotarajiwa.
“Tumewasikia viongozi wakuu wa vyama vya upinzani, tumemsikia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akitoa Altmutam wa Serikali kuwataja waliohusika na matukio na ikifika Septemba 23 wasipotajwa wao watachukua hatua
“Mtu kama Mbowe anaweza kutoa altmatam kwa Rais?Ukiona umefika hapo ujue genge la watekaji limefanikiwa, ni kazi yetu sisi na wapinzani kushirikiana kufanikisha genge la watekaji linashughulikiwa, tuasiache genge la watekaji likashinda.
“Mgombea urais wa Marekani Donald Trup alijeruhiwa kwa risasi, lakini vyama vya vyote vikubwa vinavyojitambu wote walikemea.Tunawataka vyama vya upinzani wakatae kufarakishwa na sisi kama CCM tumekataa kuingia kwenye mijadala,”amesema Dk.Nchimbi.
Amefafanua juzi wamewasikia vijana wa CHADEMA kupitia Baraza la Vijana (BAVICHA) wametoa tamko wakisema Samia must Go lakini ni vema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan yuko pale kwa Katiba na hawezi kuondoka kwa kauli ya Samia Must Go.
“Ndio maana nchi yetu inauchaguzi Mkuu kla baada ya miaka mitano ambao wananchi hupiga kura kuchagua viongozi wao.Hata ninyi mnajua Mbowe ni Mwenyekiti na Mbowe must go imeshindikana , wanamlinda wanafanya hivyo kwa Katiba yao na wameendelea kumlinda na Mbowe bado yupo.
“Hivyo Mbowe ataendelea kuwepo na Rais Samia ataendelea kuwepo.Hakuna must go.Tumesikia ndani ya CHADEMA kunampasuko na Mbowe naye ni mtuhimiwa wa mauaji hayo.Wakati Mbowe akiniambia kuhusu kutekwa kwa Ali Kibao nilikuwa namuangalia machoni lakini sioni sura ya utekaji.
“Mwingine nimemsikia mwanaharakati huru anasema John Mnyika anahusika… hivi kweli Mnyika anaweza kupanga mauaji?Mnyika hata ukimuwekea panya anakimbia, halafu leo umsingizie Mnyika anahusika.Hapana.”
VIPI KUHUSU JESHI LA POLISI ?
Akizungumza na wahariri, Dk.Nchimbi amesema kumekuwa na jitihada kubwa za kufarakanisha Jeshi la Polisi na wananchi na kwamba katika ziara wanashuhudia wananchi wanajenga vituo na wanachoomba ni kupatiwa askari, hivyo haikubaliki kuona matukio machache yakitaka kuharibu sifa nzima ya jeshi la polisi.
Amesema kuwa kati yam waka 2017 hadi mwaka 2023 Polisi ambao wameuawa katika matukio ya yaliyohusisha majambazi na kuongeza jumla ya polisi 141 wamejeruhiwa.
“Hawa polisi ambao zinafanyika jitihada ambazo zinataka kuonesha Polisi hawafai, polisi wakae dakika 24 tu tuone nini kitakachotokea.
KUHUSU WATU WALIOPOTEA
Dk.Nchimbi amesema watu waliopotea katika kipindi cha miaka mitano ni 151 na waliopatikana 141 kwa jitihada za Polisi.“Kwa hiyo kama kuna jambo ambalo halitasaidia nchi yetu ni kuwafarakanisha Polisi na wananchi kwa hiyo ni vema tukaacha kunyooshena vidole.
“Tunataka uchunguzi wa haraka ufanyike , hatua zilichukuliwe kwa watakaobainika, Chama Cha Mapinduzi kimekasirishwa sana na jambo hili, nilipopata taarifa za ule msiba.Mbowe alipopata taarifa alinipigia simu kama mara tano lakini ujasiri nilikosa, nilishindwa kupokea simu yake…
“Chama kimekasirishwa na tunaomba uchunguzi ufanyike lakini wakati tunasubiri tuwe na maamzi sahihi, juzi Geita mmeona mtu amebeba watoto wake watu wakaanza kuwahisi vibaya akakimbilia Polisi lakini watu wakaenda Polisi na kuanza kufanya vurugu.Watu wawili wamepoteza Maisha.
“Sisi kama Chama tunataka demokrasia iendelee kushamiri, mahusiano ya chama na chama yaendelee kuimarika, tuendeele kujenga nchi, tuhakikishe Watoto na wajukuu wetu waje kupata nchi nzuri.Narudia kuwaomba vongozi wa wengine watambue CCM tunaamini katika mazungumzo na wao na sisi tunawajibu wa kushirikiaana kuijenga nchi yetu, hatuna nchi nyingne.
“Tunaye Rais anayeishi kwa vitendo maridhiano, umoja na mshikamano. watanzania wote ni ndugu na tunakila sababu ya kushirikiana kujenga nchi.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...