Ashrack Miraji
MKUU wa Wilaya ya Tanga Japhari Kubecha, ameanza ziara zake za kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii, zikiwemo taasisi za kidini.
Kubecha amehamishiwa Wilaya ya Tanga akitokea wilayani Lushoto mkoani Tanga alikokuwa akihudumu kama Mkuu wa Wilaya hiyo kwa muda wa miezi mitano.
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya Kubecha amesema taasisi za dini ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamii , hivyo ameamua kufanya ziara katika taasisi hizo za dini ili kukutana na viongozi wa taasisi na kubadilishana mawazo.
Ametumia nafasi hiyo kuomba ushirikiano na kusisitiza umoja, mshikamano na maendeleo ya wilaya pamoja na kuelezea mikakati ya kuiongoza Wilaya ya Tanga.
"Nimeanza kufanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hii. Lengo langu hasa ni kutaka kujionea mafanikio ya Serikali pamoja na changamoto ambazo zinawakabili wananchi ili kuzitatua maana lengo la Serikali yetu ni kutatua changamoto kwa wananchi. "
Kuhusu ziara ambazo amezifanya mpaka sasa tangu aliporipoti katika Wilaya hiyo wiki mbili zilizopita ni kufanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo.Pia amefanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Tanga kujionea hali ya utoaji huduma.
Ametembelea machinjio ya wilaya yaliyopo Mtaa wa Sahare, Kata ya Mnyanjani na katika baadhi ya viwanda kadhaa kujionea ufanisi wake na changamoto zilizosababisha baadhi ya viwanda kutofanya kazi, na makundi ya kijamii wakiwemo wanamichezo, viongozi wa dini na wazee maarufu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...