Na Mwandishiwetu , Michuzi Tv
Mkuu wa wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo leo amefanya mkutano na wanachi wa kata nne za Kipunguni, Mzinga kitunda na kivule amabo amepata kuwaeleza namna serikali ya Rais Samia ilivyojipanga kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika kata hizo.
Aidha Dc Mpogolo ametumia wasaa huu kuwakumbusha viongozi wa kata mashina pamoja na wenye viti wa mitaa kutoa elimu ya kujiandikisha katika daftari la Wakazi hili waweze kushiriki vyema katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotaraji kufanyika mwezi wa 11.
aidha pia Dc Mpogolo ametumia mkutano huo kutoa ufafanuzi juu ya hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa DMDP ambapo amesema tayari serikali imekwishapata fedha na wakandarasi wameshapatikana kinachosubiriwa ni utekelezaji tu wa mradi huo.
''Naomb niwatoe hofu viongozi wangu serikali imejipanga katika kutekeleza mradi huu kama mnavyojua miradi aiji hewani tu lazima kuna hatua mbalimbali za kitaalamu zifuate ikiwemo Manunuzi , wakandarasilazima wafanye mobilaization na ndio sasa mtaanza kuona magreda hivyo kabla ya uchagzui wa wa serikali za mitaa miradi hii itakuwa imeanza" amesema Dc Mpogolo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...