Na Emmanuel Massaka Michuzi TV

MWENYEKITI  wa UVCCM Kata ya Mabwepande Andrew Mashimba amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu  ndani ya Chama hakuna kukatwa ambapo mshindi wa kwenda kugombea katika nafasi ya mwenyekiti wa Mtaa na wajumbe watapatikana kwenye boksi la kura.

Viongozi wote watapigiwa kura na wanachama hivyo hakuna mtu atapita Kwa  kura za mezani za viongozi kufanya kupendekeza.
Mashimba  ameyasema hayo  katika mkutano wa Wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Mbopo  jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa  kuwa wananchi wajitokeze katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kuanzia Septemba 11 hadi 20 huku wana CCM wajiandikishe ndani ya siku Nne zinatosha na sio kusubiri siku ya mwisho ya kujiandikisha.
Mashimba amesema kuwa watu wenye sifa wajitokeze kugombea awa watu wawashawishi wenye sifa ya kugombea kwani hakuna vizingizio kwamba watakatwa na viongozi wa juu.

Amefafanua kuwa  mwenyekiti wa Chama Dkt.Samia Suluhu Hassan ametangaza utaratibu mzuri wa kufanya kila mwanachama ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
Hata hivyo amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi  kuendelea kutangaza  mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika maendeleo yaliyofanyika kwenye maeneo yao.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...