KAMPUNI ya Airpay Tanzania imesema kuwa mfumo wa kidigitali walioutengeneza kwa kushirikiana na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA) na taasisi zingine za kifedha utawarahisishia wajasiriamali wa Zanzibar kupata mikopo kwa urahisi na haraka.

Hayo yamebainishwa leo na Ofisa Mawasiliano kutoka Kampuni ya Airpay Tanzania, Barnabas Mbunda wakati wa kufunga kwa Tamasha la pili la Fahari ya Zanzibar lililodumu kwa siku saba katika viwanja vya maonyesho Dimani Wilaya ya Magharibi B Unguja huku Zanzibar.

Amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na ZEEA na taasisi zingine za kifedha imewarahisishia wajasiriamali hao kupata mikopo kwa haraka na rahisi kupitia mfumo huo wa mikopo wa kidigitali.

Mbunda amesema kuwa mfumo huo utaondosha matumizi ya makaratasi kwa ajili ya kuomba na kupatiwa mikopo hivyo wajasiriamali watatumia njia ya kidigitali kupata huduma hiyo kwa haraka.

“Lengo la Airpay kuleta mfumo huu ni kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kutambulika kiuchumi ili kurahisisha kupata mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha hivyo kampuni yetu itahakikisha inawafikia wananchi wa maeneo mbalimbali Zanzinbar kwa ajili ya kuwapatia elimu namna ya matumizi ya mfumo huo,” amesema Mbunda

Akizungumzia mwamko wa wananchi katika kushiriki tamasha hilo, Mbunda amesema mwamko ni mzuri kwani wafanyabiashara na wajasiriamali wamepata fursa ya kutangaza na kuuza bidhaa zao pamoja na kupata elimu ya namna ya kufanyabiashara kidigitali.

Awali akifunga tamasha hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, Idrisa Kitwana Mustafa aliwataka ZEEA kuwawezesha wajasiriamali katika matumizi ya mfumo wa kidigitali ili kupata fursa mbalimbali za mikopo.

Amesema hatua hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali italisaidia kundi hilo kuzifikia fursa mbalimbali za mikopo na kutangaza bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje ya nchi na hatimaye kujikwamua kiuchumi.

“Mkoa wa Kusini kuna vikundi 388 vya wajasiriamali, vikundi vya kukopeshana na kulipa (sacoss)32 na vikundi vya uchumi wa buluu 229 ambavyo vinasubiri fursa za mikopo hiyo iwapo wataunganishwa na mfumo huo utawasaidia kuongeza ujuzi na kwenda na wakati katika kuendeleza biashara zao,” amesema

Kwa upande wake Arafa Hamad Bakari ambaye ni mzalishaji wa mbolea na dawa asilia, amesema Airpay imekuwa moja ya kampuni iliyotoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali juu ya umuhimu wa mifumo ya kidigitali katika kuboresha na kuendeleza biashara zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...