BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA)
inaendesha warsha ya mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi (NAOT) kwa lengo la kuhakikisha wanaendana na
mabadiliko ya viwango vya kikaguzi vya Kimataifa katika ukaguzi wao.
Warsha hiyo inajadili masuala muhimu kama viwango vya ukaguzi, utoaji wa taarifa za fedha kwa uadilifu, na matumizi ya viwango vipya vya undelezaji endelevu (sustainability) pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia katika fani ya uhasibu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno, alisema Tanzania inaongoza katika masuala ya menejimenti ya fedha za umma kwa mujibu wa Shirikisho la Wahasibu Duniani, ikishika nafasi ya kwanza pamoja na Nigeria katika utumiaji wa viwango wa kimataifa vya utayarishaji wa taarifa za fedha za umma ( IPSASs).
Aliongeza kuwa mafanikio haya yameifanya Tanzania kuwa na uwezo wa kufundisha watumishi wa serikali kutoka nchi jirani kama Msumbiji. "Hii ni taaluma pekee duniani inayofanya kazi kwa niaba ya maslahi ya umma," alieleza CPA Maneno.
Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Isaya Jeremiah, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi kwani yanalenga kuboresha utendaji wao na kuhakikisha wanakuwa na viwango vya kimataifa katika ukaguzi wa fedha za serikali.
Aliongeza kuwa mafunzo hayo yanaendana na matakwa ya Bodi ya Wakaguzi ili kuhakikisha wakaguzi wanabaki kuwa "relevant" katika taaluma yao.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Shamimu Mshana, alieleza furaha yake kushiriki mafunzo hayo, akisema kuwa yamekuwa na msaada mkubwa hasa wakati huu wa ukaguzi wa fedha za umma.
"Mafunzo haya yanatupa maarifa mapya na yanatusaidia kumwezesha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoa ripoti zenye viwango vya juu," alisema Mshana, akibainisha kuwa mafunzo hayo ni ya manufaa katika kazi zao za kila siku. 17:59

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...