OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Segerea,imewasilisha taarifa ya hali ya siasa  katika jimbo hilo ikiwa ni hatua ya kuelekea uchaguzi wa Serikali za za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Taarifa hiyo iliwasilishwa na Katibu Ofisi ya Mbunge,Lutta Rucharaba ,kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya jimbo hilo, jijini Dar es Salaam leo.

Akipokea taarifa hiyo Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya  ya Ilala , Said Sidde,alisema taarifa hiyo ni muhimu kwani inatoa  mwelekeo wa Chama katika jimbo hilo kuelekea uchaguzi ujao.

Sidde, allimshukuru Mbunge Bonnah kuandaa taarifa kwa ustadi mkubwa hali  itakayo saidia CCM kuibuka na ushindi katika jimbo  hilo.

Akiwataka wajumbe kuzingatia yaliyowasilishwa na kutimiza matakwa ya Katiba ya CCM Ibara ya 5 kwa lengo la kushinda chaguzi na kuunda serikali .

Katibu wa CCM wa Wilaya  ya Ilala, Sylivester Yared, aliwataka wajumbe kuwajibika kikamilifu katika majukumu yao kwa kubuni mbinu zitakazo saidia Chama kushinda.

Kwa upande wa Mbunge Bonnah, aliwataka wajumbe kuimarisha umoja,ushirikiano na kuongeza kasi  ya uwajibikaji.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...