Wanachama wa Vyama vya Upinzani 62 Kibaha Mji, Mkoani Pwani wamejiunga na CCM na kuahidi kuwa waaminifu na kukisaidia Chama cha Mapinduzi kikamilifu katika Chaguzi zijazo.

Vyama ambavyo wanachama hao wanatokea ni ACT WAZALENDO wanachama 40 na CHADEMA wanachama 22 ambao wameelezea kilichowashawishi ni utekelezaji wa Ilani ya CCM chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan Rais .

Akiwapokea wanachama hao ,katika Mkutano wa Viongozi wa CCM uliofanyika Ukumbi wa CCM Kata ya Mkuza Wilaya ya Kibaha Mjini, Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani ,Kitte Mfilinge amewaeleza kuwa wamefanya maamuzi sahihi.

Hata hivyo, WanaChama wa Chama Cha Mapinduzi wametakiwa kutumia vyeo vyao kwa faida ya wengine badala ya kujiona wao ni bora zaidi kwa kuwekeana mitego ya kuharibiana maisha.

Vilevile amesema wako baadhi ya viongozi wameota mapembe kwa kuwadharau wengine wakidhani kuwa wao watakaa katika nafasi hizo milele.

Kitte amesema ,dhamana ya uongozi ni kubwa na wanapaswa kuzingatia maadili katika kuwaenzi waasisi walionzisha Chama kwa maslahi ya wanachama na jamii.

Nae Silyvestry Koka Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini , amewataka wananchi wa Kibaha kumuunga mkono Rais Samia kwa juhudi anazozifanya kuinua maendeleo na Uchumi nchini.

Ameeleza, Serikali imefanya makubwa katika Taifa na Kibaha ile sio ya sasa na mwenye macho atakuwa anaona kwani kila sekta imetendewa haki kwa kuletewa mamilioni ya fedha kutekeleza miradi mbalimbali.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...