Na Mwandishi wetu Dodoma

Mkoa wa Dodoma unatarajia kuanza uboreshaji wa daftari la Kudumu la mpiga kura tarehe 25 septemba 2024 hadi tarehe 1 octoba 2024.

Uboreshaji huo ni sehemu muhimu ya mchakato wa uchaguzi na utahusisha kurekebisha taarifa waliokosa sifa,mfano waliofariki, waliofungwa kifungo cha zaidi ya miezi sita na waliopata changamoto ya afya ya akili ili kuhakikisha kuwa wapiga kura wote wanawezae kijiandikisha na kuhakiki taarifa zao.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameyabainisha hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema ni muhimu wapiga kura kuhakikisha kuwa wana taarifa sahihi ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.

RC Senyamule amesema Dodoma inakadiriwa kuwa na wapiga kura 1,777,834 kati ya hao wapo ambao hawajawahi kujiandikisha, idadi yao inakadiriwa kuwa 845,976.

"Hili ni kundi kubwa na ni kundi muhimu sana hivyo nawasihi kujitosheleza kujiandikisha" - RC Senyamule

Amesema vituo vitakavyotumika katika uboreshaji ni majengo ya umma kama vile ofisi za watendaji wa kata, ofisi za watendaji wa mitaa, ofisi za wenyeviti wa vijiji, ofisi za wenyeviti wa vitongoji na shule katika maeneo ambayo hakuna majengo ya Umma.

Aidha RC Senyamule amesema vituo vimeshajengwa na vimewekwa alama ili wananchi waweze kuvitambua na vituo hivyo ni Wilaya ya Dodoma vituo 429,Bahi 191, Kongwa 229 ma Chamwino 805.

Hata hivyo wanaohusika na zoezi hilo ni wananchi ambao

1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea
2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu mwaka 2025
3. Waliojiamdikisha awali na wamehama kata au jimbo moja kwenda kingine.
4. Waliopoteza sifa mfano waliofariki kuondolewa kwenye daftari.
5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji.
6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma amesisitiza umuhimu wae mchakato huo na amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ka uboreshaji wa daftari la Kudumu la mpiga kura.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...