Bandari ya Mtwara imeendelea kupokea Meli zaidi zinazoleta makasha matupu ambapo tarehe 27 Oktoba 2024 Meli ya MV LAKONIA ya Kampuni ya SINOTASHIP (COSCO) ilitia nanga Bandarini hapo kwa ajili ya kupakua shehena ya makasha matupu 300 na inatarajiwa kupakia shehena ya makasha 175 ya korosho za msimu wa mwaka 2024/2025.

Meli hii ni ya pili kuletwa na Kampuni ya SINOTASHIP baada ya MV CONTSHIP DAY kutia nanga tarehe 1 Oktoba 2024 ikiwa na makasha matupu 240.

Meli hii inafanya jumla ya Meli zilizowasili katika Bandari ya Mtwara kufikia nane (8) ambapo inafanya idadi ya makasha matupu yaliyowasili hadi sasa kufikia 3,999 tayari kwa kuanza kuhudumia shehena ya korosho kwenda nchi za nje.

Aidha, Meli ya MV LAKONIA itakuwa ya kwanza kwa msimu huu kuanza kusafirisha korosho ghafi kwenda nchi za nje ambapo itasafirisha korosho hizo kwenda nchini Vietnam.

Kampuni ya SINOTASHIP imeahidi kuendelea kuleta Meli nyingine ikiwemo MV AREOPOLIS inayotarajiwa kutia nanga mwanzoni mwa mwezi Novemba ikiwa na makasha matupu 300.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...