Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Getrude Mbiling’i (kulia) akimuelekeza mteja kujaza fomu ya malalamiko kuhusu huduma zinazodhibitiwa na EWURA katika viwanja vya Shule ya Msingi Uyui Tabora ikiwa ni sehemu ya maadhimishk ya Wiki ya Huduma kwa Mteja iliyoanza iliyoanza leo Oktoba 7,2024.



Watumishi wa EWURA Kanda ya Magharibi wakikata keki kuashiria kuanza kwa Wiki ya Huduma kwa Mteja, mjini Tabora leo Oktoba 7,2024.



Watumishi wa EWURA katika picha ya pamoja tayari kuwahudumia wananchi na wadau wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja, iliyoanza leo Oktoba 7,2024.

Na.Mwandishi Wetu.

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi imepokea, kusikiliza na kutatua malalamiko ya wateja yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA katika sekta za nishati(umeme, mafuta, gesi asilia) na maji na usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja yaliyoanza leo 7/10/24.

Kaimu Meneja wa Kanda hiyo, Mha. John Kitonga amesema EWURA itatoa huduma hiyo kwa wateja kwa wiki nzima ( 7-11 Oktoba 2024) katika viwanja vya shule ya Msingi Uyui,manispaa ya Tabora ili kuwafikia wateja wenye uhitaji wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.

“Wateja na wadau wetu,tembeeleni banda la EWURA hapa Uyui mpate huduma za moja kwa moja za utatuzi wa malalamiko, maombi ya leseni na vibali vya ujenzi,changamkieni fursa hii”. Alilisitiza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...