Farida Mangube, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima amewataka watanzania kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa maono yake ya kuwa na uchaguzi huru na wahaki nyakati zote ili kulinda tunu ya umoja, amani na upendo aliyeiacha kiongozi huyu.

Rc Mlima amesema hayo wakati akifungua Kongamato la 21 la kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere lililoandaliwa na Chuo kikuu Mzumbe na kubeba kauli mbiu isemayo “Mtazamo wa Mwl. Nyerere juu ya dhana ya uchaguzi huru na wa haki”.

Amesema mtazamo wa Mwalimu kuhusu uchaguzi huru na wa haki si suala la kisiasa tu, ni suala la kulinda rasilimali watu ambayo kutoka miongoni mwao, wanapatikana viongozi na watendaji bora, watakao tunga sera na sheria bora zitakazo ongoza Taifa.

Aidha amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe kuandaa watu wenye maadili na sifa nyingine za kiongozi bora ili kuwezesha uwepo wa utawala bora utakaotunza rasilimali za Taifa kwa maendeleo endelevu ya Taifa hili.

Kwa upande wake Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Pro. William Mwegoha amesema kwa miaka mingi, Chuo Kikuu Mzumbe tumekuwa na utaratibu wa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya makongamano ya kitaaluma yanayojadili mitazamo tofauti ya Mwalimu Nyerere, ikiwemo utawala bora, mchango wa vyuo vikuu katika kuboresha kilimo biashara, na uchumi mzunguko kwa maendeleo ya Taifa,

Amesema Chuo Kikuu Mzumbe kwa mwaka 2024 imekuja na kauli "Mtazamo wa Mwalimu kuhusu Dhana ya Uchaguzi Huru na wa Haki." ikiwa ni mahsusi nyakati hizi ambapo Taifa linakaribia kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa mwezi Novemba, na uchaguzi mkuu hapo mwakani 2025.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...