Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linamshikilia mtuhumiwa mmoja mkazi wa Buruma wilaya ya mbinga kwa kosa la kumnyonga mwenza wake aliyefahamika kwa jina la Marcelina Erasto na kuchoma moto chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco Chilya wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema tukio hilo limetokea kwenye nyumba ya kulala wageni ya Maleta iliyopo wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma, majira ya saa tatu za usiku.
Hii ni mara baada ya chumba walichofikia wawili hao kuonekana kinawaka moto tukio lililopelekea majirani kwenda kutoa msaada wa kuzima moto huo hivyo wakati wanaendelea na zoezi la kutoa msaada ndipo walipogundua kulikua na mtu alikua amelala chooni na mwenza wake akiwa hayupo.
Baada ya kufanya upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma walibaini kua mtuhumiwa alikuwa na wivu wa mapenzi hivyo kupelekea kumnyonga mwenza wake na kuchoma godoro kwa lengo la kupoteza ushahidi kitendo kilichopelekea kuteketea kwa baadhi ya vitu mbalimbali na mpaka sasa mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma (SACP) Marco Chilya amezungumzia mafanikio ambayo jeshi la polisi wameyapata kutokana na opereseheni zinazoendelea kufanyika mkoani Ruvuma.
Amesema Mnamo tarehe 7.11.2024 majira ya saa sita na nusu mchana kijiji cha lilondo kata ya wino halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T 185 EBX aina ya Toyota Dayna Truck ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Frank Ndunguru likitokea Songea kwenda Njombe akiwa na mwenzake Nickson James (29), Mfanyabiashara mkazi wa mtaa wa Buswelu wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.
Ambapo walikamatwa wakisafirisha dawa za mifugo aina tofautitofauti zizadhaniwazo kua ni bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi millioni 78
Na mara baada ya kufanya uchunguzi jeshi la polisi kwa kushirikiana na timu ya wataalamu wa ukaguzi wa dawa (TMDA) ilibainika kua dawa hizo zimeingizwa nchini kinyume cha sheria na kwamba baadhi ya dawa ni bandia na nyingine zikiwa chini ya kiwango.
Aidha katika kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27/11/2024 Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma kupitia jeshi la polisi ametoa wito kwa wananchi wote watakaoshiriki zoezi la uchaguzi, jeshi la polisi linawahakikishia usalama wa kipindi chote cha kampeni kabla na baada ya uchaguzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...