NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari mkoani Dar es Salaam kuhusu mikopo ya mtandaoni, lengo likiwa ni kuongeza ufahamu wa jamii kuhusu masuala yanayohusu mikopo hiyo.
Akizungumza wakati akifungua Mafunzo hayo leo Novemba 14, 2024 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Huduma Ndogo za Fedha, Dickson Gama amesema BoT itaendelea kuhakikisha sekta ya fedha inakuwa thabiti, imara na stahimilivu ili kuwawezesha shughuli za uchumi zinapatikana kwa wakati.
"Ni jukumu la BoT katika kusimamia huduma Ndogo za fedha nchini hivyo kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari kiunganishi kati ya Benki Kuu na jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla,"Amesema
Ameeleza kuwa mikopo ya mitandaoni imekuwa ni sehemu ya mfumo wa fedha kwani imerahisisha utoaji wa huduma za mikopo kwa urahisi zaidi na haraka.
Amesema ukuaji huo wa haraka umesababisha changamoto kadhaa ikiwemo masuala ya kimaadili, riba kubwa gharama kubwa za mikopo na kukosekana kwa taarifa.
Pamoja na hayo amesema kutokana na changamoto hizo wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ili kufanya huduma hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi na mtoa huduma kuidhinishwa na BoT.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...