Na Oscar Assenga,TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt Batilda Burian amesema kwamba katika mkoa huo wana vituo 5,405 ambavyo vitatumika kupigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika kesho huku akieleza vifaa vyote vimekwisha kwenda kwenye maeneo yote.
Dkt Burian aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi huo ambapo alisema kwamba na maeneo yote ambayo yatatumika kwenye upigaji wa kura wameshayakagua na utayari upo.
Alisema kwamba anaamini watu wa Tanga ni waastaarabu na wasiotaka fujo waende kupiga kura wakijua kwamba Tanga ni ya amani na Tanzania ni ya amani.
“Twendeni tukapige kura kwa sababu muda wa kupiga kura ni mchache kuliko tuliotumia kwenye uandikishaji na vituo vya kupiga kura vitafunguliwa asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili jioni ingawa saa 10 ndio muda wa mwisho kufika kituoni hivyo nawasihi wananchi tutumie fursa ya kupiga kura ili tuweze kuchangua viongozi”Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo kama walivyofanya wakati wa zoezi la uandikishaji ili kupata watu wengi kupiga kura na kuweza kufikia malengo ambayo wanayategemea kama mkoa wanataka zoezi liwe kubwa watu wote waweze kushiriki.
“Lakini Katika mchakato mzima wa rufaa zilizokuwepo ni 298 katika hizo zilizorejeshwa ni 264 na rufaa 34 zilizoshindwa kurejeshwa kutokana na kukosekana vigezo vya kikanuni vya kuruhusu rufaa hizo ziweze kupitishwa ”Alisema
Aidha alisema rufaa 264 ambazo zimepitishwa nyengine ni katika kusaidia watu wote washiriki kwenye uchaguzi huo huku akieleza mambo ya hitilafu mbalimbali za makosa ya kiuandishi mengi yalivumiliwa ili kuweza kuona wanakuwa na demokrasia nzuri na vyama vyote vinashiriki kwene uchaguzi huo.
Hata hivyo alivitaja vyama ambavyo vitashiriki kwenye uchaguzi huo kuwa ni CCM,ACT,CUF,Chadema,NCCR ,NLD,SAUTI na hao ndio wengi wamesimamisha wagombea pamoja na uwepo wa vyama vyengine kama UDP na vyengine zinavyofahamika nchini.
“Katika Mkoa wetu huu tuna Vijiji 763, vitongoji 4528, mitaa 270 na katika Halmashauri 11 ,miji midogo mitatu Mombo wilaya ya Korogwe, Lushoto na Muheza lakini pia tuna Jumla ya Kata 245 "Alisema
"Katika kipindi cha uandikishaji, hatua ya mchujo na kwenda kwenye kampeni hatujapata changamoto yoyote ile sio kwenye vyama vya siasa hiyo yote ni kuhakikisha tunakwenda kwenye uchaguzi tukiwa wamoja na kusonga mbele lakini niwashukuru wote waliojitokeza kwenye zoezi la uandikishaji ambapo Tanga iliibuka kidede namba mbili kwenye zoezi la uandikishaji .
“Tuliweza kuvuka lengo la uandikishaji tulitegemea kuandikisha watu Milioni 1.4 lakini tumekwenda kuandikisha watu milioni 1.6 na kupelekea Mkoa kuwa asilimia 110.9 nawapongeza wananchi ,wanahabari kwa jinsi mlivyopeleka habari na hamasa na hamasa kubwa iliyochochea mwitikio kwa wananchi kwenda kujiandikisha”Alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...